Mvua yaleta balaa uwanja Russia

Muktasari:

  • Miongoni mwa sehemu zilizoathirika ni mji wa Volgograd ambako mafuriko ya Mto Volga, yamesababisha tope kufunika barabara na eneo lote kuuzunguka uwanja wa Volgograd, moja ya viwanja vilivyotumika katika mechi za fainali za Kombe la Dunia.

VOLGOGRAD, Russia.  Mvua kubwa zilizonyesha jana katika maeneo mbali mbali ya Russia zimesababisha mafuriko na uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu.

Miongoni mwa sehemu zilizoathirika ni mji wa Volgograd ambako mafuriko ya Mto Volga, yamesababisha tope kufunika barabara na eneo lote kuuzunguka uwanja wa Volgograd, moja ya viwanja vilivyotumika katika mechi za fainali za Kombe la Dunia.

Volgograd Arena, uwanja unaochukua watazamaji 45,000, ulitumika katika mechi za makundi ukiwemo mchezo ambao England iliifunga Tunisia mabao 2-1.