SportPesa inavyoupiga mwingi katika maendeleo ya michezo nchini
Huwezi kuzungumzia maendeleo ya soka nchini ndani ya miaka mitano iliyopita bila kutaja mchango wa kampuni namba moja ya michezo ya kubashiri Afrika MasharikiSportPesa.
SportPesa sio kwamba tu wameleta mapinduzi katika sekta ya michezo ya kubahatisha nchini kutokana na machaguo mengi ya michezo hiyo lakini pia imekuja kubadilisha sekta nzima ya michezo.
Kuanzia udhamini wa vilabu vya ligi kuu Tanzania Bara, kudhamini mashindano matukio mbalimbali ya kimichezo, kuleta timu kubwa za Ulaya kuja kucheza mechi Tanzania (Sevilla na Everton) nk.
Hakika wanastahili kupewa “maua yao”. Mbali na juhudi hizo Sportpesa pia imekuwa ikishiriki kwa kiasi kikubwa katika ukarabati na uboreshaji wa miundombinu ya michezo nchini.
Katika uboreshaji wa miundombinu, SportPesa ni moja ya wadau wakubwa ambao walitenga kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa ili kuboresha miundombinu mbalimbali ya uwanja huo.
Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni Tanzania ilipewa heshima na Shirika la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa muandaaji wa mechi ya ufunguzi ya michuano mipya ya African Super League ambapo mchezo huo wa ufunguzi utawakutanisha Simba ya Tanzania na Al Ahly ya Misri.
Mapema mwaka huu, Serikali ilitangaza kuanza utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya taa za uwanjani, mifumo ya umeme, vyoo na mifumo ya uokoaji, mifumo ya Tehama, vyumba vya kubadilishia nguo, mabango ya matangazo ya wadhamini na mengine mengi.
Kwa kuwa mchezo wa soka unavuta hisia za watu wengi duniani, hatua ambayo Serikali ya Tanzania imeipiga ni muendelezo wa jitihada za wadau za kukuza maendeleo ya sekta ya michezo nchini ambapo itakumbukwa kampuni kinara wa michezo ya kubashiri Afrika Mashariki, SportPesa ilishafanya jambo kama hilo mwaka 2018, ikiwa ni mdau wa kwanza kufanya hivyo.
SportPesa ilitenga kiasi cha Sh1.4 bilioni kwa ajili ya kufanya ukarabati wa miundombinu ya uwanja huo baada ya kupita kipindi cha miaka 10 ya shughuli za michezo bila ya kufanyiwa maboresho yoyote tangu ufunguliwe rasmi mwaka 2007.
Maboresho hayo yalihusisha eneo la kuchezea, vyumba vya kubadilishia nguo kwa wachezaji na waamuzi na miundombinu mingine muhimu.
Hii yote ni katika kuhakikisha sekta ya michezo hususani mchezo wa soka ambao unavutia Watazamaji wengi kuvutia wadhamini wengi ambao watakuwa na uhakika wa kupata faida ya uwekezaji wao ili kuendelea kulinda heshima na hadhi hiyo ambayo Taifa letu imepata.
Bado nchi yetu inaihitajiSportPesa katika kuhakikisha inaendelea kusaidia kuboresha miundombinu ya michezo ilivopo nchini ambayo bado ipo katika mandhari nzuri lakini inaweza kukidhi matakwa ya michezo ya mashindano ya ndani kama vile ligi na kombe la shirikisho ili kutoa nafasi ya ushindani wa kweli katika ligi na kujenga uchumi wa vilabu kwa kuvutia wawekezaji zaidi.