Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Toto African yaiharibia Simba SC

Winga wa simba Shiza Kichuya (kulia) akimtoka beki wa Toto African,Carlos Protas wakati wa mchazo wa ligi kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye uwanja wa CCM kirumba Jijini Mwanza jana.Timu hizo zilitoka suluhu.Picha na Michael Jamson

Muktasari:

Mara ya mwisho Simba kuifunga Toto kwenye uwanja huo ilikuwa 2010 na tangu hapo imeambulia vipigo au sare.

Dar/Mikoani. Toto African imeiharibia Simba kwa kuipunguza kasi katika mbio za ubingwa msimu huu baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza jana.

Mara ya mwisho Simba kuifunga Toto kwenye uwanja huo ilikuwa 2010 na tangu hapo imeambulia vipigo au sare.

Simba ilihitaji ushindi katika mchezo huo ili kuendelea kuiacha mbali Yanga kieleleni, lakini kwa matokeo hayo imeendelea kuizidi kwa pointi sita huku wakiwaachia faida ya mechi mbili mkononi.

Vilevile matokeo hayo yanazidisha ugumu kwa Simba kutangazwa bingwa mapema kwani, Simba imebakisha mechi tatu na ikishinda zote itakuwa na pointi 71 sawa na Yanga.

Yanga ikishinda mechi hizo itafikisha pointi hizo lakini inajivunia magoli ya kufunga. Simba ina mabao 44 wakati Yanga ina mabao 50 kibindoni.

Mechi ilivyokuwa

Timu zote zilianza mchezo kwa kasi huku Simba ikionekana kupwaya katikati licha ya kumchezesha James Kotei, Mzamiru Yassin na Mohamed Ibrahim, lakini ikazidiwa na viungo wa Toto, ambao walionekana kutawala eneo hilo.

Toto ilikuwa ya kwanza kufika langoni kwa Simba na dakika ya 16, Juvenary Pastory aliikosesha bao timu yake baada ya mpira wake wa kichwa kudakwana kifundi na kipa wa Simba Daniel Agyei.

Simba ilijibu mashambulizi dakika ya 18, lakini Laudit Mavugo alikosa bao la wazi baada ya kupiga shuti lililotoka nje.

Timu hizo ziliendelea kukosa mabao kwani dakika ya 26, Japhary Mohammed alikosa bao baada ya kuachia shuti kali nje kidogo ya 18 na kupaa juu ya lango, huku Fredirick Blagnon wa Simba akikosa bao dakika ya 34, baada ya kuwapiga chenga mabeki wa Toto, lakini akapiga fyongo na mpira kutoka nje.

Simba iliendelea kukosa mabao licha ya kufika mara nyingi langoni kwa Toto hasa dakika 10 za mwisho za kipindi cha kwanza kupitia kwa Shiza Kichuya, Mavugo na Blagnon na kwenda mapumziko zikiwa suluhu.

Timu hizo zilirudi mapumziko huku Simba wakilisakama zaidi lango la Toto kupitia kwa Ibrahim Ajib, Blagnon lakini uimara wa kipa Mussa Mohammed na mabeki wake Ramadhan Malima na Yusuph Mlipili uliisaidia timu hiyo kukwepa kipigo.

Baada ya mchezo huo, wachezaji wa Toto wakiongozwa na kocha wao, Novatus Fulgence waliungana na mashabiki wanaodhaniwa kuwa wa Yanga kushangilia sare hiyo.

Kwenye Uwanja CCM Mkwakwani mkoani Tanga, Azam FC ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na JKT Ruvu.

Azam ilikuwa ya kwanza kufunga dakika ya 15 kupitia kwa Shaaban Iddi aliyetumia udhaifu wa mabeki wa JKT Ruvu waliokuwa wakitegeana kumkaba mfungaji kabla ya Mussa Juma kuisawazishia JKT Ruvu dakika ya 26 kwa kichwa.

Frank Nchimbi aliiongezea JKT bao la pili, lakini Erasto Nyoni akaisawazishia Azam FC kwa shuti kali nje ya 18 na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare.

Kwenye Uwanja wa Mlandizi, Pwani, Ruvu Shooting iliipa kipigo Majimaji cha mabao 4-1.

Mabao ya washindi yalifungwa na Abdulrahman Mussa aliyefunga ‘hat trick’ huku lingine Majimaji ikijifunga, wakati bao la wageni likifungwa na Alex Kondo.

Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, Stand United imetoka suluhu na Mtibwa Sugar.