Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Twiga Stars kuanza kibarua WAFCON

Muktasari:

  •  
  • Kwa mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye WAFCON ya mwaka 2010 ambapo Twiga Stars ilipangwa kundi moja na Mali, Afrika Kusini na Nigeria

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars leo itashuka kwenye  Uwanja wa Stade Municipal de Berkane nchini Morocco, kuivaa Mali katika mchezo wa kwanza wa kundi C kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON).


Michuano hiyo inayofanyika nchini Morocco ilianza rasmi juzi kwa mchezo wa kundi A, ambapo timu mwenyeji Morocco ilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Zambia na jana kulikuwa na mechi nyingine kadhaa ambapo Senegal ilivaana na DR Congo, Nigeria ikacheza na Tunisia huku Algeria ikivaana na Botswana.

Twiga Stars ni miongoni mwa timu 12 zinazoshiriki fainali hizo za WAFCON na leo inaanza safari yake kwa kuminyana na Mali katika kundi gumu lililojumuisha pia mabingwa watetezi Afrika Kusini na Ghana.

Licha ya kukosa huduma ya mshambuliaji wake anayeichea Brighton ya England, Aisha Masaka, aliyepata majeraha ya paja bado safu ya ushambuliaji ya Stars ina mastaa kama Clara Luvanga (Al Nassr), Opah Clement, Stumai Abdallah na kinda Jamila Rajabu (JKT Queens) ambao wote wana uwezo wa kubadili matokeo ya mchezo.

Kwa mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye WAFCON ya mwaka 2010 ambapo Twiga Stars ilipangwa kundi moja na Mali, Afrika Kusini na Nigeria. Katika mchezo dhidi ya Mali, Stars ililala kwa mabao 3-2, mabao ya Mali yalifungwa na Aicha Konate, Diarra na N'Diaye ambao kwa sasa hawapo kwenye kikosi huku mabao ya Tanzania yakifungwa na Sophia Mwasikili, kwa sasa meneja wa Simba Queens na Fatuma Swalehe.

Miaka imepita na sasa vikosi vyote viwili vimejaa na damu changa, huku Twiga Stars ikijivunia kikosi kipya chenye wachezaji wenye vipaji kuanzia safu ya ulinzi hadi ushambuliaji.

Matumaini ya Watanzania wengi yapo kwa Clara Luvanga, mshambuliaji mwenye nguvu, akili na uwezo mkubwa wa kuliona lango la wapinzani  akitarajiwa kuwa mhimili muhimu kwenye mchezo huo.

Kocha wa Twiga Stars, Bakari Shime, amesema “Tupo kwenye kundi lenye timu ngumu, hususan Mali ambao wamewahi kushiriki mara kadhaa michuano ya WAFCON, na bila kusahau Afrika Kusini, mabingwa watetezi. Mchezo hautakuwa rahisi hata kidogo."

"Kiakili tuko vizuri kuelekea kwenye mashindano haya. Tumefanya maandalizi ya kutosha na kila kitu kiko sawa. Tunaamini tutapata matokeo mazuri, na tunawaahidi Watanzania wote kuwa tutapambana kwa ajili yao."