Twiga yabeba ubingwa wa Cosafa

Saturday October 09 2021
ushindipic
By Mustafa Mtupa

TIMU ya taifa ya Wanawake 'Twiga Stars’ imefanikiwa kuchukua ubingwa wa Cosafa baada ya kuifunga Malawi bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa Port Elizabethi huko Afrika ya Kusini.

Twiga imefanikiwa kuchukua ubingwa huo kwa mara ya kwanza tangu ianze kualikwa na mwaka pekee iliowahi kufanya vizuri ilikuwa 2011 ambapo ilimaliza nafasi ya tatu.

Goli la Tanzania lilifungwa dakika ya 64 na Enekia Kasonga ambaye katika siku za hivi karibuni timu yake ilimuuza kwenda Morocco katika klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco 'AUSFAZ'

Mechi hiyo ilionekana kuwa ngumu kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho kwani mbali ya Twiga kushinda Malawi ilionekana kulisakama vyema lango lao lakini umakini ulisababisha wasipate nafasi ya kusawazisha.

Tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo ilichukuliwa na Kapteni wa Twiga Amina Bilal ambaye pia alichukua tuzo ya mchezaji bora wa mashindano.

Advertisement