Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ugonjwa uliokatisha uhai wa Kocha Bilo hadharani

Mashehe wakiwa katika ibada ya kusalia mwili wa Aliyekuwa Kocha wa Billo Queens, Athuman Bilali nyumbani kwake Nyasaka jijini Mwanza.

Muktasari:

  • Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 17, 2026, CEO wa Bilo Qeens, Lawrence Mapunda, amesema madaktari hospitalini wamesema kifo cha Kocha Athuman Bilali kilisababishwa na presha.

Mwanza. Imetajwa kuwa Kifo cha aliyekuwa kocha wa Bilo Queens Athuman Bilali ‘Bilo’ kimesababishwa na presha ya ghafla.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 17, 2026, CEO wa Bilo Qeens Lawrence Mapunda, amesema madaktari hospitalini walisema kifo chake kilisababishwa na presha.

“nilipewa taarifa kuwa kocha yupo eneo la michezo na nilimkuta amedondoka. Tulipomfikisha hospitalini nilishtuka kuambiwa amefariki na nilikuwa nawaza nani atashika hii nafasi.  Nafasi hii iko wazi na tutafanya mpango jinsi gani ya kuiziba.

“Kwa mujibu wa madaktari umauti wake kilichosababisha tulicholetewa wamesema tu ni presha,” amesema Mapunda.

Anasema siku hiyo walikuwa na mipango ya kukutana katika uwanjani na yeye ndiye aliyekuwa mtu anayetakiwa akutane naye kwa ajili ya kupanga mipango ya safari ya timu.

Kituo cha Bilo Football kilianzishwa na Bilali Athumani kwa lengo la kuwasaidia wachezaji waliokataliwa na makocha kwa madai ya kutokuwa na vipaji, wachezaji waliokatazwa kucheza mpira na wazazi wao na kilikuwa fursa kwa makocha wasiokuwa na kazi kufundisha timu hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Saidi Mtanda akiwa katika mazishi ya Athuman Bilali kwenye makabuli ya Nyasaka katika jijini Mwanza.

“Shauku yake kubwa ilikuwa lazima tuwe na uwanja, tukiamishe kituo kiwe cha michezo na hadi sasa tuna kiwanja karibia hekari sita eneo la Kisesa kwa sababu eneo tulilopo ni la serikali.

“Na mipango mingine ilikuwa ni kufikia mwakani lazima tuwe tumepata gari ya kusafiria ya timu ndiyo aliyotuachia na tutayaendeleza,” amesema Mapunda.

Mchezaji wa Mwana Stars Veterans, Mwemezi Mushumbausi, amesema mafanikio yalifanywa na Bilali ni pamoja na kuipandisha timu kwenda Ligi Kuu ya Wanawake.

Mapunda ameongeza kuwa malengo yao yalikuwa ni makubwa sana na vitu ambavyo vilikuwa hawa vifahamu watu ni pamoja na mikakati ya ujenzi wa kiwanja cha timu hiyo

Mtoto wa Bilo, Hamisi Bilali amesema wao kama watoto wake na familia yao kiujumla watayaendeleza yale ambayo baba yao ameyaacha.

“Ugumu upo hata kipindi baba yupo, hatuna budi kuvaa gwanda na kulipambania hili swala maana moja ya ndoto yake ni kuanzisha kituo kikubwa na chenye mafanikio, na amekuwa akituhusisha katika hili kujua namna ya kuendesha kituo hiki,” amesema mtoto huyo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amesema wadau wa mpira wa miguu waache kuwa na maneno maneno bali wawe na vitendo katika kuunga mkono michezo.

“Mashabiki wengi wa mpira ni watu wamaneno si watu wa vitedo, nio watu wa kulaumu lakini sio watu wa msaada, wanapenda matokeo lakini hawana mchango katika hayo matokeo,” amesema Mtanda.

Pia amehaidi atachangia kiasi cha Sh5 milioni  kwa ajili ya kusaidia jitihada zake na amenunua basi kwa ajili ya timu ya Bilo kutumia endapo watakuwa na mchezo wowote nje ya Mwanza.

Mbunge wa Ilemela, Dkt Angeline Mabula amewaasa wapenzi wa soka waiendeleze timu hiyo ya soka kwani haitopendeza kama timu hiyo itaishia njiani.

“Niwaombe wapenzi wa soka timu hii haitakiwi ibaki yatima. Wadau wa mpira kwa ujumla wa kike kwa wa kiume na viongozi wote, sifa aliyoiacha Bilo timu yetu kushiriki katika Ligi Kuu ni sifa ya mkoa na wilaya,” alisema Mabula.

Wanachezaji wa Billo Queens wakiwa katika mazishi ya aliyekuwa Msimamizi na mlezi wao Athumani Bilali nyumbani kwake Nyasaka jijini Mwanza.

Naye mwenyekiti wa chama cha wananchi CAFU, Milambo Kamili ameiomba serikali kupitia jitihada alizozifanya Bilo iongeze nguvu katika kuwekeza kwa vituo vya michezo vya kukuza vipaji vya watoto wa kike.

Bilo katika uhai wake amefundisha timu kadhaa ikiwamo Toto Africans aliyoichezea pia, Gwambina FC, Alliance FC na hadi anakutwa na umauti alikuwa mmliki wa kituo cha michezo cha Bilo Sports chenye timu ya Bilo Queens ya Ligi Kuu ya Wanawake.