Wachezaji 25 Azam wawafuata JKT Tanzania

AZAM FC wametangaza majina ya wachezaji 25 waliosafiri leo Jumatano Aprili 14, 2021 kuelekea Dodoma kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa 26 dhidi JKT Tanzania mechi iliyopangwa kuchezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Kupitia kwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Thabit Zakaria maarufu 'Zaka Zakazi' ameweka wazi majina ya wachezaji hao 25 pamoja na benchi la ufundi lenye jumla ya watalamu sita.
Wachezaji hao ni Wilbol Maseke, Benedict Haule, Mathias Kigonya, Braison Rafael, Prince Dube, Nico Wadada, Abdul Haji Omar 'Hamahama, Bruce Kangwa, Paschal Msindo, MudathirYahya, Aubrey Chirwa na Never Tigere.

Wengine ni Danny Amoah, Abdallah Kheri Sebo, Ally Niyonzima, Idd Suleiman Nado, Awesu Ally Awesu, Ayoub Lyanga, Yakubu Mohamed , Ismail Aziz Kader, Agrey Morris, Mpiana Monzinzi, Emmanuel Kabelege, Yahya Zayd, na Salum Abubakary 'Sure Boy'.
Pia viongozi wa Benchi la Ufundi waliosafiri ni Kocha mkuu George Lwandamina, Kocha msaidizi Vivier Bahati, Kocha wa makipa Idd Abubakary, Mtaalamu wa viungo Nyasha Charandura na Madaktari wa timu wawili Mwanandi Mwankemwa na
Luckson Kakolaki.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani kwani Azam walio nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi na alama 47 watahitaji ushindi ili wazidi kuwasogelea vinara Yanga wenye alama 51 huku JKT Tanzania walio nafasi ya 13 na alama 27 watahitaji ushindi utakao wasogeza hadi nafasi ya 12.
Kwa mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikua Octoba 30 kwenye mchezo wa Ligi kuu na zilitoka sare ya bao 1-1.