Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasajiliwa dakika ya 90, Djuma akwama

Dar es Salaam. Dirisha kubwa la usajili kwa Tanzania limefungwa rasmi juzi, huku nyota kadhaa wakisajiliwa saa chache kabla ya kufungwa kwake.

Coastal Union ilifunga usajili kwa kunasa saini za nyota wawili wa kigeni ikianza na kipa Ley Matampi kutoka DR Congo na beki Konare Malienne raia wa Mali.

KMC nayo ilikuwa haijamaliza usajili hadi pale ilipoinasa saini ya kiungo wa kimataifa wa Somalia, Abdukarrim Qubaaye kutoka katika klabu ya Horseed ya nchini kwao.

Pamba ya Mwanza inayoshiriki Championship iliwasajili wakali wawili wa Ligi Kuu, Hassan Mwasapili aliyewahi kuwika na Mbeya City pamoja na kipa Shaban Kado akitokea Ihefu FC.


Djuma akwama

Wakati hao wakipenya kwenye usajili katika dakika za mwisho, beki wa zamani wa AS Vita na Yanga, Djuma Shabani alijikuta akikwama kutua Azam FC baada ya kipa Mcomoro, Ali Ahmada kuweka ngumu.

Azam FC ilikuwa tayari kumsajili Djuma na alikuwa ameanza mazoezi na Wanachamazi hao, lakini juzi ikakwama baada ya kipa Ahmada kugoma kuondoka.

Azam ilitaka kumtoa Ahmada ili nafasi yake aingie Djuma lakini kipa huyo aligoma kwa kile alichohofia kukosa timu kwani madirisha mengi ya usajili yamefungwa.

Kwa maana hiyo, kugoma kuondoka kwa Ahmada kuliifanya Azam FC kuwa na wachezaji 12 wa kigeni, ambao wanahitajika kwa kanuni za TFF, hivyo Djuma kubaki njia panda na sasa anatafuta mpango mwingine.