Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga uwanjani kuivaa Ihefu mpya

Muktasari:

  • Ihefu FC, imefanikiwa kuifunga Yanga misimu miwili mfululizo, baada ya msimu uliopita pia kuichapa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Highland Mbarali Mbeya, lakini ilipotua Dar es Salaam, ilichapwa bao 1-0.

Yanga leo jioni inaingia uwanjani tena kwenye mechi kali ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu, ikitaka kulipa kisasi baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Ihefu FC, imefanikiwa kuifunga Yanga misimu miwili mfululizo, baada ya msimu uliopita pia kuichapa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Highland Mbarali Mbeya, lakini ilipotua Dar es Salaam, ilichapwa bao 1-0.

Mechi hiyo pekee kwa leo itapigwa kuanzia saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, ambao wenyeji hawajapoteza katika michezo minane iliyocheza hapo msimu huu, lakini wakiwa na kiu ya kutaka kulipa kisasi cha kipigo ilichopewa na wageni wao katika mechi ya duru la kwanza msimu huu ukiwa ndiyo mchezo pekee waliopoteza.

Ihefu iliitungua Yanga katika mechi hiyo ya kwanza iliyopigwa Oktoba 4, mwaka jana, kikiwa ndicho kipigo pekee alichokutana nacho Kocha Miguel Gamondi katika Ligi Kuu tangu ajiunge na timu hiyo.

Takwimu zinaonyesha katika mechi tano zilizopita kwa timu hizo zilipokutana katika Ligi tangu mwaka 2020, Ihefu imeshinda mbili za nyumbani na kupoteza moja ilipofumuliwa 3-0, huku ikipoteza michezo miwili ya ugenini,kitu ambacho huenda leo ikaikabili Yanga ili kutaka kulivua joho la unyonge mbele ya wenyeji wao hao wanaongoza ligi.

Yanga ambayo leo itaendelea kukosa huduma za baadhi ya nyota tegemeo akiwamo kiungo Khalid Aucho ambaye ameripotiwa kufanyiwa upasuaji, itaikabili Ihefu likiwa ni pambano la 18 kwao msimu huu na la tisa ikiwa nyumbani.

Baada ya ligi kurejea Februari 2, Yanga imecheza mechi sita, ikishinda tano mfululizo, moja ikitoka suluhu kwa upande wa Ihefu inayowategemea nyota wapya waliotua kupitia dirisha dogo kutoka Singida FG, kama Elvis Rupia, Duke Abuya, Marouf Tchakei, Joash Onyango na kipa Abubakar Khomeiny, yenyewe imeshinda mechi tatu, ikapoteza moja na sare moja.

Katika michezo 10 ya ugenini Ihefu imeshinda mara mbili tu na nyingine kama hizo ikitoka sare, huku sita ikifungwa, imefunga mabao 10 na kuruhusu nyavu zao kuguswa mara 16 na kuvuna pointi nane kati ya 30, ilizopaswa kubeba kupitia mechi hizo.Kazi ya ulinzi:

Mabeki wa Yanga wakiongozwa na nahodha Bakar Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Nickson Kibabage na Yao Kouassi watakuwa na kazi wa kuwachunga kina Rupia, Abuya, Tchakei na wengine wasimtungue kipa atakayeanza langoni, japo ukuta huo unaonekana ni mgumu kwani katika mechi tano zilizopita umeruhusu mabao mawili tu na kwa jumla kwenye ligi umeruhusu mabao tisa.

Hata hivyo, kwa namna safu ya ushambuliaji wa Ihefu ikiongozwa na Tchakei na Rupia ilivyoweka rekodi ya kufunga walau bao moja kwenye kila mchezo kati ya mitano iliyocheza itawafanya kina Bacca kuwa makini.

Ihefu kupitia mechi tano zilizopita za Ligi Kuu, imefunga mabao manane, japo ukuta wao umeruhusu mabao sita kitu kinachoweza kuwa msala kwao wanapokutana na safu kali ya ushambuliaji ya Yanga inayoongozwa na Mudathir Yanga aliyefunga mabao matano katika mechi tano zilizopita ikiwa na wastani ya kufunga bao moja kila mchezo.

Pia kuna nyota wengine tishio eneo la ushambuliaji akiwamo Clement Mzize na kinara wa mabao wa timu hiyo, Stephane Aziz KI mwenye mabao 11, moja pungufu na aliyonayo Feisal Salum 'Fei Toto' anayeongoza orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu hadi sasa.

Mabeki wa Ihefu wakiongozwa na Onyango, Benson Mangolo, Faria Odongo na Benjamin Tanimu au Lenny Kissu aliyeitungua Yanga kwenye mechi zote za jijini Mbeya zilizopita watakuwa na kazi ya kuwazuia nyota wa Yanga wasiendelee moto wa kugawa vipigo vinono kama ilivyofanywa na timu nyingine ilizokutana nazo Chamazi kwa jumla timu hiyo ikiwa imefunga mabao 42.

Yanga inahitaji ushindi leo ili kuzidi kupanua pengo la pointi baina yao na Azam iliyopo nafasi ya pili na kwa watani wao Simba iliyowazidi pointi saba hadi sasa.

Yanga inaongoza msimamo ikiwa na pointi 46 baada ya mechi saba na kama itashinda itafikisha 49, kwani Azam ina pointi 44 kwa sasa lakini ikicheza michezo 20, wakati Simba yenye 39 imecheza mechi 17 na kesho itarudi uwanjani kukabiliana na Singida FG katika mfululizo wa michezo wa ligi hiyo iliyoingia raundi ya 21 kwa sasa. Yanga inasaka taji la tatu mfululizo baada ya kulibeba mara mbili.

Kwa upande wa Ihefu matokeo mazuri kwao yatawatoa katika nafasi ya nane hadi kuingia Sita Bora, kwani itaifanya ifikishe pointi 26. Kwa sasa ina 23 kupitia mechi 19 ilizocheza na kocha wa timu hiyo, Mecky Maxime amekiri hiyo ni mechi ngumu kutokana na kasi ya Yanga, lakini ameandaa timu ili kupata matokeo mazuri ugenini.

Tunafahamu mchezo ni mgumu, lakini tumeiandaa timu kupata ushindi kwenye mechi hii," alisema Mecky.

Kwa upande wa Gamondi, akizungumzia mchezo huo wa leo alikaririwa akisema; "Kwetu kila mechi ni muhimu na tunataka kushinda. Tunajua Ihefu ndio timu pekee iliyotujeruhi msimu huu leo ni siku nzuri ya kulipiza kisasi hiki, wachezaji wanafahamu, benchi la ufundi tunafahamu na tunaamini tutapata alama tatu."