Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yanusa nusu fainali CAF, Mayele kama kawaida

TIMU ya Yanga imeanza vyema hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Godswill Akpabio.

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza uliopigwa nchini Nigeria, shujaa wa Yanga aliyeipa furaha ni mshambuliaji nyota wa timu hiyo, Fiston Mayele aliyefunga mabao yote mawili dakika ya 73 na 81.

Katika michezo 15 ya CAF ambayo Rivers imecheza ikiwa nyumbani huu unakuwa ni mchezo wa pili kwao kupoteza baada ya awali kufungwa bao 1-0 na Far Rabat ya Morocco ikishinda 12 na sare dhidi ya Disables Noirs.

Miongoni mwa timu ambazo Rivers imewahi kuzifunga ikiwa nyumbani ni Enyimba, Club Africain, Asec Mimosas, El Merrick, Wydad Casablanca na Bloemfontein.

Katika michezo 11 iliyopita ya mashindano ya Klabu Afrika ambayo Rivers United imecheza nyumbani imeshinda minane, sare miwili na kupoteza mmoja ikifunga jumla ya mabao 33 na kuruhusu manane.

Kwa upande wa Yanga katika michezo 11 ikicheza ugenini imeshinda mitano, sare mmoja na kupoteza mitano ikifunga mabao 11 na kuruhusu 10.

Yanga imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali kwani katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Aprili 30 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam inahitaji sare tu.

Endapo Yanga itafuzu hatua hiyo itakutana na mshindi kati ya Pyramids (Misri) au Marumo Gallants ya Afrika Kusini.