Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yapewa mwamuzi wa bahati dhidi ya AS FAR

Muktasari:

  • Mara ya mwisho Yanga kuchezeshwa na mwamuzi huyo ilikuwa Januari 4, 2025 ambapo iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe.

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limemteua mwamuzi, Ahmad Imtehaz Heerallal kuchezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utaikutanisha Klabu ya Yanga dhidi ya AS FAR ya Morocco, Novemba 22, 2025 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Katika mchezo huo wa kundi B ambao Yanga itakuwa nyumbani, inaonekana kubebwa na rekodi za mwamuzi huyo ambaye hadi sasa ameshachezesha jumla ya mechi 48 za mashindano mbalimbali ya CAF yanayozijumuhisha timu za Taifa pamoja na Klabu.

Katika mechi hizo 48, Imtiaz ametoa jumla ya kadi 120 ambapo ametoa nyekundu mbili wakati za njano akiwa ametoa 118 ikiwa ni wastani wa kutoa kadi tano kila baada ya mechi mbili. Mwamuzi hiyo raia wa Mauritania katika michuano ya Klabu za CAF amechezesha jumla ya michezo 14 akitoa kadi za njano 30 na nyekundu moja.

Bahati kwa Yanga

Yanga inaonekana kuingia na bahati ya mwamuzi katika mechi ya Jumamosi kwani katika mechi 14 alizochezesha, timu mwenyeji zimeshinda mara nane ikiwemo Yanga yenyewe ambayo ilichezeshwa na mwamuzi huyo Januari 4, 2025 na iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Ni timu moja pekee ambayo ndiyo iliyoambulia kipigo ilipokuwa nyumbani ikichezeshwa na mwamuzi huyo ambayo ni Stade d'Abidjan ya Ivory Coast iliyokubali kipigo cha bao 0-1 dhidi ya CR Belouzidad ya Algeria Desemba 7, 2024, wakati michezo mitano ikiisha kwa timu za nyumbani kutoka sare.

Simba ni miongoni mwa timu zilizopitia kipigo ilipokuwa ugenini dhidi ya mwamuzi huyo kwani ilikubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Raja Casablanca, Machi 31, 2023 kwenye Uwanja wa Mohamed wa tano, Morocco.

Hivyo basi, licha ya kubebwa na rekodi ya mwamuzi, Yanga inatakiwa kuhakikisha inajiandaa vizuri kuwakabili AS FAR ili kuondoka na pointi tatu za nyumbani na kujiweka sehemu nzuri katika kundi B ambalo linaonekana kuwa gumu kutokana na ushindani wa timu zilizopo za Al Ahly, AS FAR, na JS Kabylie kwani kila moja inataka kwenda robo fainali.