Yanga yathibitisha Fei Toto kutua Azam
Muktasari:
BAADA ya mgogoro wa muda mrefu kati ya Klabu ya Yanga na mchezaji wao Feisal Salum 'Feitoto' ni rasmi sasa wamemaliza mgogoro huo na kumuuza kwenda Azam FC.
BAADA ya mgogoro wa muda mrefu kati ya Klabu ya Yanga na mchezaji wao Feisal Salum 'Feitoto' ni rasmi sasa wamemaliza mgogoro huo na kumuuza kwenda Azam FC.
Taarifa hiyo imetolewa leo kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano ya mitandao ya kijamii ya klabu hiyo na kueleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
Taarifa imeeleza kuwa Feisal ameuzwa kwa dau ambalo halitawekwa wazi kutokana na makubaliano ya pande zote mbili.
"Uongozi wa Yanga unapenda kuutarifu umma kuwa umepokea ofa kutoka katika klabu ya Azam FC ya kumuhitaji Feisal Salum na baada ya makubaliano ya pande zote mbili uongozi umefikia uamuzi wa kumuuza mchezaji huyo kwa klabu ya Azam FC," ilieleza taarifa hiyo