Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

'Kopa Maji' ya TCB kuboresha upatikanaji wa huduma za maji safi na usafi wa mazingira

Mkurugenzi wa Huduma za Wateja Wadogo na Biashara wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Henry Bwogi (katikati) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya ‘Kopa Maji.’Wanaoonekana kulia na kushoto kwake ni maofisa waandamizi wa benki hiyo.

Dar es Salaam. Agosti 2023, Benki ya Biashara nchini (TCB) ilizindua huduma ya mkopo wa maji, ijulikanayo 'Kopa Maji' ikilenga kutatua changamoto zinazoikabili Tanzania hususan katika upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira.

Huduma hiyo bunifu ya kifedha inakwenda kuwasaidia Watanzania kuwa na miradi ya maji ya uhakika na ubora wa huduma za usafi wa mazingira, inayohusisha uunganishwaji na huduma ya maji, uchimbaji wa visima na unyonyaji taka kutoka katika vyoo.


Utanuaji wigo wa huduma za kifedha kupitia bidhaa

Mikopo ya 'Kopa Maji' imebuniwa kutoka kwenye jalada pana la bidhaa za kifedha la Benki ya TCB. Wateja wanaweza kupata huduma hii kupitia njia mbalimbali ikiwamo; mikopo ya kibiashara, mikopo ya kampuni (taasisi), mikopo ya wateja, mikopo midogo na mikopo midogo ya nyumba.

Zoezi la uenezaji wa huduma mpya ya ‘Kopa Maji’ maeneo ya vijijini likiendelea kushika kasi.

Hatua hii ya utanuaji wigo wa upatikanaji wa huduma zake ni tafsiri ya azma ya benki ya kutaka kufungamanisha huduma za maji na usafi wa mazingira na zile za kifedha.


Jitihada za kutekeleza malengo mbalimbali ya nchi na dunia

Hatua hii inaunga mkono moja kwa moja Sera ya Taifa ya Maji na inatekeleza kwa vitendo lengo namba 6 la Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG), ambalo linasisitiza upatikanaji wa maji safi na huduma za usafi wa mazingira kwa wote.

Kwa kuliangalia eneo hilo, TCB si kwamba tu inachangia uimar¬ishaji wa afya za watu na ustawi wao nchini bali pia inachangia moja kwa moja katika uchumi wa nchi kwa kuwashika mkono watu wenye viwanda vidogo na vya kati (SMEs) ambao wanachangia walau asilimia 30 ya Pato la Taifa.

Kuwezesha wajasiriamali wadogo na kati (SMEs) na kukuza ukuaji uchumi

Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Adam Mihayo, katika kauli yake ya hivi karibuni, alisema kuwa benki imeweka mkakati mahsusi wa kuwawezesha wajasiriamali wadogo na kati kupitia msaada wa kifedha.

TCB ina mpango wa kugawa mikopo yenye thamani zaidi ya Sh300 bilioni kwa wajasiriamali wadogo na kati ndani ya mwaka 2024, uwekezaji mkubwa ambao utaimarisha uwezo wa biashara nyingi kiundeshaji na kuchangia katika ukuaji mkubwa wa kiuchumi na uzalishaji wa fursa za ajira.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Adam Mihayo akizungumza na waandishi wa habari mwanzoni mwa mwaka huu.

Rekodi za faida ya benki zinaakisi uimara wa taasisi hiyo kifedha

Mwenendo wa kifedha wa benki umeonekana kuiamarika maradufu kwa kupata faida baada ya kodi ya Sh10.7 bilioni ndani ya robo ya kwanza ya mwaka 2024. Faida hii si tu inafafanua uimara wa benki hiyo kifedha sokoni bali inapigia mstari uwezo wake wa kuchangia miradi mbalimbali ya kijamii kama vile ili¬vyofanya katika 'Kopa Maji.'


Mipango ya siku za usoni

Kupitia kampeni ya 'Kopa Maji', TCB inatarajia kuwezesha zaidi ya Watanzania 61,000 kupata hudu¬ma ya maji na usafi wa mazingira kufikia mwaka 2025, ikiwa ni seh¬emu muhimu ya uboreshaji wa afya ya umma na hali ya maisha kwa ujumla.

Bidhaa hizi mahsusi za kifedha zinaonyesha kwa vitendo namna gani zinaweza kusaidia kutatua changamoto za kijamii na kuongo¬za njia kwa sekta nzima ya benki kuziendea changamoto kama hizo kwa kuzigeuza kuwa fursa.

TCB inaendelea kutumia vyema msingi wake wa uimara wa kifedha sokoni kuwezesha utekelezwaji wa miradi ya kijamii ambayo inaunga mkono vipaumbele vya kitaifa na malengo endelevu ya dunia.  Kupitia 'Kopa Maji,' TCB sio tu taasisi ya kifedha, bali ni mshirika muhimu wa maendeleo na ustawi wa Watanzania.