Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baba Levo aahidi barabara za lami kupatikana hata kwa ‘uchawa’

Muktasari:

Mgombea ubunge Kigoma mjini Clayton Chipando maarufu Baba Levo, amesema endapo akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha anapambania miundombinu ya barabara na kufufua masoko yaliyokufa.


Kigoma. Mgombea ubunge Kigoma Mjini, Clayton Chipando maarufu Baba Levo (CCM), amesema wananchi hao endapo wakimpa ridhaa ya kuingia bungeni atahakikisha analeta barabara za kiwango cha lami katika mji huo kwa njia yoyote ikiwa kwa kuomba, uchawa au kufoka na kwamba hawezi kuahidi ahadi ambazo hawezi kutimiza.

Akizungumza leo Jumatatu, Septamba 22, 2025 katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Kitongoni, Baba Levo amesema hawezi ahidi ahadi ambavyo hawezi kutimiza yeye sio sifa yake kusema uongo kwa wananchi.

Baba Levo amesema akishindwa kuleta barabara katika kipindi chake, akienda tena kuomba kura mwaka 2030 wamfukuze kwani hawezi ahidi SGR wakati anajua hawezi kutumiza.

Amesema wananchi hao wakimchagua mbali na kuboresha miundombinu ya barabara ataboresha masoko ya jioni na kuwa ya kisasa likiwemo soko la kwa Noti, Gungu na Marungu.

“Suala la kwenda kuisemea Kigoma Mjini, ni mimi ndiye naweza, hakuna mtu anayenizidi mdomo nitawaelewesha wasiwafungie wananchi Ziwa Tanganyika, nitaleta barabara za kiwango cha lami pamoja na masoko ya jioni, hivyo nichagueni mimi ninatosha,”amesema Baba Levo.

“Mimi napenda sifa sana hivyo nitahakikisha naboresha masoko, najenga masoko na kufufua soko la ujiji ili nikiwa napita wanisifie pia kuweka taa, pevament na meza mpya za kuweka bidhaa zenu na si kuweka chini,”amesema Baba Levo

Mgombea Udiwani Kitongoni, Himid  Mkunda amesema Kigoma mjini inahitaji mabadiliko na kwamba hakuna mabadiliko bila kuichagua CCM.

Amesema wakati anaomba kura kuwa diwani wa Kata ya Kitongoni mwaka 2020 kwa mara ya kwanza, aliahidi zahanati kwenye kata hiyo na ametimiza hiyo ahadi na sasa inafanya kazi.

Amesema alisimamia kama diwani na wakapata madarasa 12 kwa fedha za uviko 19 na matundu ya choo kwa wanafunzi wa kiume.

“Magati yote ya kata hiyo yalikuwa hayatoi maji kwa kutumia gharama zangu nimerudisha maji na kujenga magati mengine. Nimefanya zaidi ya haya hivyo nipeni tena ridhaa ya kuwa diwani niendelee kuleta maendeleo zaidi,”amesema Mkunda.

Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Haruna Kambilo amesema kuna maneno mengi yanaendelea mtaani likiwemo mgombea wao wa ubunge kuwa siyo msomi, lakini chama hicho kina taratibu zake za kuchagua mgombea hivyo wameona anatosha na ndio maana wakamchagua aweze kugombea jimbo hilo.

“Kigoma Mjini hatuhitaji mbunge msomi kwani tulishawahi kuwa na msomi, usomi sio sifa ya kiongozi na wananchi tulio wengi hapa siyo wasomi hivyo tarehe 29 twende tukachague mtu ambaye siyo msomi mwenzetu ili aweze kutembea na shida zetu na kututetea ,”amesema Kambilo.