Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barabara yenye kiwango cha lami yajengwa Mwenge, Lindi

Barabara yenye urefu wa mita 600 yenye kiwango cha lami iliyopo mtaa wa Mwenge imewekwa jiwe la msingi na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Wazo Mwang'onda. Picha na Bahati Mwatesa

Muktasari:

  • Barabara ya Bohari yenye urefu wa mita 600 ya kiwango cha lami yajengwa mtaa wa Mwenge Manispaa ya Lindi lengo likiwa kuongeza mtandao wa barabara za lami katika Manispaa hiyo.

Lindi. Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inaendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa mita 600 katika Mtaa wa Bohari, Kata ya Mwenge  Manispaa ya Lindi.

Mradi huo unaotekelezwa kwa fedha za Mfuko wa Mafuta (Fuel Levy) unagharimu zaidi ya Sh466 milioni ukiwa na lengo la kuboresha miundombinu ya usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Wazo Mwang'onda Meneja wa TARURA Wilaya ya Lindi, Mhandisi Dawson Paschal amesema kuwa mkandarasi anayetekeleza mradi huo ni kampuni ya SEC ya Mtwara, ambapo amesema kuwa ujenzi huo ulianza Septemba 20, 2024 na unatarajiwa kukamilika Mei 28, 2026.

"Hadi sasa mradi huu umefikia asilimia 90 na kazi zilizofanyika ni kusafisha eneo la barabara, kujenga tabaka la msingi pamoja na uwekaji wa mifereji na makalavati ili kuhakikisha barabara hiyo inadumu kwa muda mrefu,"amesema Mhandisi Paschal.

Aidha, TARURA imebainisha kuwa kati ya mita 600 zinazotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami, kipande cha mita 510 kinaendelea kutekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha.


Mhandisi Paschal ameeleza  kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa, kupunguza changamoto ya vumbi pamoja na kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa wakazi wa Kata ya Mwenge  na maeneo jirani.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa, Mwang'onda akiweka jiwe la msingi amewapongeza TARURA kwa jitihada za usimamizi mzuri wa miradi ya barabara na kuwataka kuongeza juhudi kumalizia sehemu iliyobaki ikiwemo kuweka taa za barabarani.

"Nawapongeza TARURA kwa kazi kubwa ya usimamizi wa miundombinu ya barabara niwaombe kumaliza kwa wakati ikiwemo taa za barabarani ili wananchi waweze kutembea usiku na mchana." amesema Mwang'oka.

Asha Juma mkazi wa kata ya Mwenge ameishukuru Serikali kwa ujenzi wa barabara hiyo kwani awali walikuwa wanapata shida sana hasa kipindi vja mvua.

"Naishukuru Serikali kwa juhudi kubwa waliyoifanya kwa kutuwekea lami katika barabara hii kwani tulikuwa tunateseka sana kipindi cha mvua, huwezi kupita kwa bodaboda ni lazima utembee kwa miguu maana hakuna chombo kinachofika huku."amesema Juma

Mwenge wa uhuru Manispaa ya Lindi umekimbizwa kilomita 35 miradi saba yenye thamani ya Sh720 milioni imekaguliwa, kuonwa, kuwekewa mawe ya msingi na kuzinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa.