Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ya wapangaji jengo lililoanguka K’koo yahamishiwa Usuluhishi Mahakama Kuu

Wafanyabiashara 50 waliokuwa wamepanga vyumba vya biashara katika jengo lililoanguka katika mtaa wa Mchikichini na Kongo, eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam mwaka 2024, ambao wamefungua kesi ya madai dhidi ya wamiliki wa jengo hilo wakidai fidia wakiwa nje ya jengo la Mahakama Kuu Kituo cha Usuluhishi.

Muktasari:

  • Novemba 16, 2024 jengo la ghorofa lilianguka katika mtaa wa Mchikichi na Kongo, eneo la Kariakoo, na kusababisha vifo vya watu 31.Hata hivyo wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara ndani ya jengo hilo walifungua kesi wakidai fidia ya jumla ya Sh40 bilioni

Dar es Salaam. Kesi ya madai ya wafanyabiashara waliokuwa wamepanga vyumba vya biashara katika jengo lililoanguka katika mtaa wa Mchikichini na Kongo, eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam mwaka 2024, sasa itasikilizwa Machi 30, 2026 Mahakama Kuu Kituo cha Usuluhishi.

Kesi hiyo ya madai imefunguliwa na Kanali Naftal Swai, Sultan Dibwe, Dicko Marcus Msigwa, Aurelian Aloyce Msigwa,  Christina Elias Snga pamoja na wenzao wengine 45,  dhidi ya wamiliki wa jengo hilo wakidai fidia ya jumla ya Sh40 bilioni.

Wadaiwa katika kesi hiyo ni Zenabu Abdallah Ismail (mwakilishi wa marehemu Ismail Abdallah Salim), Ashour Awadh Ashur (mwakilishi wa marehemu Awadh Ashour Abeid), Leondela Augustino Mdete na wenzako watatu.

Awali, kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi na ilikuwa inasikilizwa mbele ya Jaji Mohamed Gwae.

Hata hivyo, kwa kuwa kesi hiyo haikuanzia katika hatua ya usuluhishi, Jaji Gwae alielekeza shauri hilo lipelekwe Mahakama Kuu Kituo cha Usuluhishi ili pande zote mbili zifanye usulushihi.

Jaji Gwae, wakati anaahirisha kesi wiki iliyopita, alitoa siku 30 kwa pande zote zikae pamoja na kufanya usuluhishi na kama itashindikana kufikia muafaka katika siku hizo alizotoa, basi kesi hiyo itarudishwa kwake.

Jengo hilo lililojengwa katika Kiwanja Na. 12, Block 7, eneo la Kariakoo, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, lilianguka Novemba 16, 2024.

Hata hivyo, Novemba 29, 2024, wamiliki wake walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na kusomewa kesi ya kujaribu kuua.

Washtakiwa hao katika kesi hiyo ya jinai ni Leondela Mdete(49) mkazi wa Mbezi Beach,  Soster Nziku(55) mkazi wa Mbezi Beach, Aloyce Sangawe(59) mkazi wa Sinza na Stephen Nziku(28) mkazi wa Mbezi beach.

Katika kesi hiyo uchunguzi wa awali namba 33633/2024, walisomewa mashtaka 31 ya kuua bila kukusudia kinyume cha vifungu vya 195 na 198 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu (PC). kutokana na vifo vya watu hao wakidaiwa kutenda makosa hayo.

Wanadaiwa kuwa Novemba 16, 2024 katika mtaa wa Mchikichi na Kongo, eneo la Kariakoo, washtakiwa hao isivyo halali walishindwa kutimiza majukumu yao na kusababisha vifo vya Said Juma na wenzake 30.

Kwa sasa kesi hiyo imehamishiwa Mahakama Kuu kwa taratibu za usikilizwaji kamili, baada ya upelelezi kukamilika na washtakiwa kusomewa hoja za awali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. 

Wakati wamiliki wa jengo hilo wakipandishwa kizimbani kwa kesi hiyo ya jinai, waliokuwa wapangaji katika jengo hilo wao walifungua kesi ya madai Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi kabla ya kuamuriwa kupelekwa kwenye usuluhishi.

Wafanyabiashara waliokuwa wamepanga vyumba vya biashara katika jengo lililoanguka katika mtaa wa Mchikichini na Kongo, eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam mwaka 2024, wakiwa katika Mahakama Kuu Kituo cha Usuluhishi, baada ya kesi yao kuahirishwa. Picha na Hadija Jumanne

Leo Jumanne, Machi 17, 2026 kesi hiyo imetajwa kwa mara ya kwanza Mahakama Kuu, Kituo cha Usuluhishi na imepangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Zahra Maruma.

Wakati kesi hiyo ilipotajwa, Jaji Maruma alikuwa na anasikiliza mashauri mengine, hivyo kesi hiyo iliahirishwa na Naibu Msajili wa Kituo cha Usuluhishi, Augustina Mmbando hadi Machi 30, 2026.

“Kwa hiyo, leo kesi ilikuwa imepangwa kwa Jaji Maruma ambaye leo alikuwa anasikiliza mashauri mengine yanaendelea, hivyo kutokana na hali hiyo ameipangia tarehe nyingine ambayo ni Machi 30, 2026”, amesema Mmbando na kusisitiza

“Na siku hiyo wadawa na wadaiwa wote wanatakiwa kuhudhuria kesi bila kukosa kama nyaraka zenu zinavyoonyesha mahakamani hapa.”

Akiwafafanulia wateja wake kuhusiana na hatua hiyo, wakili wa wadai, Daniel Yona ambaye alimwakilisha Peter Madeleka amesema kuwa usuluhishi huo ni kwa mujibu wa sheria ambayo inahitaji kwanza kabla ya kesi kusikilizwa lazima usuluhishi ufanyike.


 Madai ya kesi ya msingi:

Katika kesi hiyo, wadai hao wanaiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wawalipe jumla ya Sh40 bilioni kama fidia ya hasara ya uwekezaji na biashara.

Wanadai kuwa hasara hiyo ilisababishwa na uzembe wa wadaiwa kwa ujenzi wa sakafu ya chini ya ardhi usioruhusiwa uliofanywa na wadaiwa, kinyume na makubaliano ya upangaji kati yao na wadaiwa uliosababisha jengo hilo kuporomoka.

Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo, kwa nyakati tofauti kuanzia Januari 2023 hadi Desemba 31, 2024, wadai na wadaiwa waliingia katika mikataba (kwa mdomo na kwa maandishi) ya kupanga katika jengo hilo.

Walalamikaji, wakiwa wapangaji wa wadaiwa, waliwekeza na kuendesha biashara mbalimbali yakiwemo maduka ya rejareja na ya jumla katika jengo hilo.

Jumla ya thamani ya uwekezaji na biashara za wadai zilizokuwa zinaendeshwa katika jengo hilo ni Sh40 bilioni.

Wanadai kuwa kwa kuvunja masharti na vigezo vya mikataba wa upangaji kati yao wadai na wadaiwa, wadaiwa walifanya kwa uzembe ujenzi wa chini ya ardhi bila idhini ya mamlaka husika.

Hali hiyo wanadai kuwa ilisababisha kuporomoka kwa jengo hilo Novemba 16, 2024, na kuwasababishia hasara ya uwekezaji na biashara zao wadai ndani ya jengo hilo.

Wanadai kuwa wamekuwa wakidai mara kwa mara wadaiwa wawalipe Sh40 bilioni kama fidia kwa hasara hiyo ya uwekezaji na biashara yao, iliyosababishwa na uzembe wa wadaiwa katika ujenzi huo, uliosababisha kuporomoka kwa jengo hilo.

Hivyo wanaiomba mahakama itamke kuwa wadaiwa, kwa kuvunja mikataba ya upangaji kati yao na wadai, walifanya kwa uzembe na bila idhini ujenzi huo wa jengo hilo na kusababisha hasara kwa uwekezaji na biashara zao wadai zilizokuwa zinaendeshwa ndani ya jengo hilo.

Pia wanaomba malipo  ya fidia maalum kiasi cha jumla ya Sh40 bilioni, malipo ya fidia ya hasara ya jumla kwa kadri mahakama itakavyotathmini, hgarama za kesi na nafuu nyinginezo ambazo mahakama itaona zinafaa.

Hata hivyo leo wanadai kuwa wadaiwa katika kesi hiyo walikuwepo mahakamani hapo na Naibu Msajili Mmbando amewasisitiza Machi 30, 2026 wawepo mahakamani hapo kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi hiyo.