Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kijiji cha Bima chazinduliwa Sabasaba

Kamishna wa Bima, Dk Baghayo Saqware (katikati) akizindua rasmi shughuli za Kijiji cha Bima katika maadhimisho ya Miaka 50 ya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam maarufu Sabasaba. Wengine ni viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tira) na watendaji wakuu wa kampuni mbalimbali za bima.

Muktasari:

  • Imeelezwa kuwa, kukua kwa sekta ya bima kunategemea sana uelewa wa wananchi kuhusiana na dhana nzima ya bima

Dar es Salaam. Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tira) imezindua rasmi shughuli za Kijiji cha Bima katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam maaraufu (Sabasaba).

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumamosi Julai 7, 2026 ikiongozwa na Kamishna wa Tira, Dk Baghayo Saqware na kuhudhuriwa na viongozi wa kampuni za bima, madalali wa bima, watoa huduma na wadau mbalimbali wa sekta ya bima hapa nchini.

Dk Saqware amesema kukua kwa sekta ya bima kunategemea sana uelewa wa wananchi kuhusiana na dhana nzima ya bima.

Kwa mujibu wa taarifa ya Tira, Kijiji cha Bima ni jukwaa la kila mwaka linaloratibiwa na Tira kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya bima kwa lengo la kuwasogezea wananchi elimu ya bima, ushauri wa kitaalamu na huduma mbalimbali za bima katika eneo moja.

Kupitia jukwaa hilo, wananchi hupata fursa ya kujifunza umuhimu wa kuweka bima aina mbalimbali kwa lengo la kulinda maisha, afya, mali, biashara na uwekezaji wao kwa jumla.

Dk Saqware amesema jambo hilo linahitaji ushirikiano mkubwa wa wadau wote katika kuhakikisha elimu na huduma za bima zinawafikia Watanzania wengi zaidi.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kutembelea kijiji hicho cha bima kilichozinduliwa ili kupata elimu sahihi inayohusiana na masuala yote ya bima pamoja na kuwa nafasi ya kuchagua aina ya bima watakazozihitaji.

Kwa mujibu wa taarifa ya uongozi wa Tira katika kipindi chote cha maonyesho, wananchi watapata huduma za ushauri, elimu ya bima, ufafanuzi wa bidhaa mbalimbali za bima pamoja na nafasi ya kukutana ana kwa ana na kampuni zinazojishughulisha na huduma za bima pamoja na wadau wengine walioko kwenye sekta hiyo.

Dk Saqware amesema ushiriki wa Tira Sabasaba unaendana na dhamira ya kuongeza uelewa wa umma kuhusu bima katika kukuza ujumuishi wa huduma za kifedha na kuimarisha mchango wa sekta ya bima katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.

“Uongozi wa Tira unaendelea kuhimiza wananchi kutumia huduma za bima kama nyenzo muhimu ya kudhibiti vihatarishi na kujenga ustahimilivu wa kifedha kwa watu binafsi, biashara na taasisi,” amesema.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jubilee, Harold Adamson amesema maonesho haya yamewasaidia kusogea karibu na wateja wao na kutoa elimu zaidi kuhusu huduma zao.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Strategis ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya shughuli zote za Kijiji cha Bima, Kelvin Mushi amewapongeza watendaji wa kampuni mbalimbali ya bima kwa kuunga mkono kuanzishwa Kwa Kijiji cha Bima.