Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maandamano yatikisa Rawalakot, waandamanaji wadhibitiwa

Wanaharakati nchini Pakistan wamezitaka mamlaka nchi humo kushughulikia kero mbalimbali zinazotolewa na wananchi, si kutumia nguvu kuzuia maandamano hali inayosababisha vurugu na hata mauaji.

Wameeleza hayo kutokana na vurugu zinazoendelea Rawalakot ambao ni mji mkuu wa wilaya ya Poonch uliopo katika eneo kubwa la Kashmir.

Wananchi katika eneo hilo wanaandamana wakipinga msako dhidi ya wanaharakati wanaodaiwa kuwa wajumbe wa kamati ya pamoja ya amani ya Jamuu na Kashmiri (J&KJAAC).

‘’Mvutano uliongezeka baada ya mamlaka kutangaza J&KJAAC kuwa shirika lililopigwa marufuku. Viongozi wa maandamano wanadai huduma za intaneti zilisitishwa kuanzia usiku wa Juni 5 na hivyo kuzuia mawasiliano kwa kiasi kikubwa katika eneo lote,’’

‘’Machafuko yalizidi kufuatia ripoti kwamba wanachama wawili wa J&KJAAC ambao ni Shahzaib Habib na Amjid Kashmiri waliuawa wakati wa makabiliano yanayohusiana na maandamano yanayoendelea,’’ alisema Liz Shariff, mmoja wa wanaharakati nchini Pakistan.

Shariff alisema vifo hivyo vimekuwa sababu ya waandamanaji kuongezeka na kuishutumu mamlaka kutumia nguvu nyingi dhidi ya wanaharakati.

‘’Maandamano yataendelea kulingana na ratiba licha ya vikwazo vya usalama vilivyoongezeka. Haya ni madhara ya kuzuia kila jambo hata kama ni haki ya watu kikatiba,’’ alidai Shariff.

Taarifa zinaeleza kuwa maandamano hayo yameenea hadi nje ya Rawalakot ambapo watu wamezuia njia kwa kuweka matairi barabarani na kusababisha shughuli mbalimbali kusimamia kwa muda.

Katika kuhakikisha usalama unaimarika, askari wamesambazwa katika maeneo mbalimbali, huku wanaharakati hao wakitaka nguvu isitumike na badala yake waachiwe wawasilishe kilio chao kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu.