Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashambulizi ya Iran, Israel yapandisha zaidi bei ya mafuta

Hofu ya kuongezeka kwa mgogoro wa Mashariki ya Kati imeendelea kuyumbisha soko la mafuta duniani, baada ya mashambulizi mapya kati ya Iran na Israel kusababisha bei ya mafuta kupanda kwa zaidi ya asilimia 4 ndani ya siku moja.

Mwenendo huo unakuja wakati soko likiwa tayari limeathiriwa na tetesi na hofu kuhusu usalama wa Mlango wa Hormuz, eneo linalochukuliwa kuwa na umuhimu mkubwa katika usafirishaji wa nishati duniani.

Katika siku chache zilizopita, bei ya mafuta ilipanda hadi takribani dola 104 kwa pipa kutokana na wasiwasi wa uwezekano wa kukwama kwa usafirishaji kupitia Strait of Hormuz, kabla ya kushuka hadi karibu dola 95 baada ya kuibuka kwa matumaini ya mazungumzo na kupungua kwa mivutano.

Hata hivyo, matumaini hayo yameonekana kufifia haraka kufuatia mashambulizi mapya yaliyoripotiwa, hali iliyosukuma tena bei ya mafuta kuelekea dola 99 kwa pipa katika masoko ya kimataifa.

Wachambuzi wa sekta ya nishati wanasema changamoto kubwa kwa sasa si upatikanaji wa mafuta duniani, bali hatima ya usalama wa Mlango wa Hormuz ambao hupitisha takribani asilimia 20 ya mafuta yanayosafirishwa kwa njia ya bahari duniani.

Iwapo njia hiyo itazuiliwa au kukumbwa na changamoto za kiusalama, athari zake zinatarajiwa kujitokeza kwa kasi kwenye bei za mafuta, gharama za usafirishaji na hatimaye kupandisha bei za bidhaa mbalimbali duniani.

Kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, ambazo hutegemea mafuta kutoka eneo la Ghuba ya Uajemi, hali hiyo inaendelea kufuatiliwa kwa karibu huku wataalamu wakionya kuwa endapo vita vitaendelea au kusambaa zaidi, shinikizo la bei linaweza kuongezeka katika miezi ijayo.

Mwenendo wa siku za karibuni unaonyesha jinsi soko la mafuta linavyosukumwa zaidi na matukio ya kisiasa na kijeshi, ambapo kila dalili ya utulivu hushusha bei na kila mivutano mipya huirudisha juu kwa kasi.