Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtiania UDP aahidi kuwajaza ‘mapesa’ Watanzania, asisitiza haki kwenye uchaguzi

Mtiania wa urais kupitia Chama cha UDP, Saum Rashid akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi za INEC baada ya kuchukua fomu ya urais.

Muktasari:

  • Msafara wa mgombea urais wa UDP umeingia saa 3:30 asubuhi akiwa na watu wachache waliokuwa wakiimba nyimbo zenye mahadhi ya moja ya makabila yanayotoka Kanda ya Ziwa.

Dodoma. Mtiania wa urais kupitia Chama cha UDP, Saum Rashid ameibuka upya na sera ya kuwajaza mapesa Watanzania, iliyoasisiwa na mwenyekiti wake, John Cheyo, akisema sasa ndiyo wakati wake.

Saum ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Agosti 15, 2025 baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kwenye nafasi hiyo.

Msafara wa mgombea huyo uliingia saa 3:30 asubuhi akiwa na watu wachache waliokuwa wakiimba nyimbo zenye mahadhi ya moja ya makabila yanayotoka Kanda ya Ziwa.

Hata hivyo, amejitofautisha na wagombea wengine kwa namna alivyoingia na wapambe wake kwani ukiacha CCM, huyu ni mgombea mwingine aliyekuwa na wasindikizaji watu wazima wake kwa waume.

Wazee waliovalia sare nyeupe za chama hicho wameonekana kuwa na nyuso za furaha na wakiimba nyimbo kwa sauti zao bila kutumia vyombo saidizi.

Hata baada ya kukabidhiwa fomu hizo, waliondoka kwa mbwembwe wakiwa na wagombea wao eneo la ofisi za INEC.

“Watanzania watupe nchi ili tukawajaze mapesa, tunavyo vipaumbele vingi lakini hili la mapesa muhimu sana,” amesema Saum.

Ametaja njia zitakazopelekea watu kujazwa na manoti ni kuboresha miundombinu ikiwemo ya kilimo, viwanda na masuala ya biashara ili kuvusha nchi katika matatizo ya kiuchumi.

Amewataka INEC kutenda haki na kuacha kukatakata majina ya wagombea ili kila mwenye haki na sifa apewe kuwaongoza Watanzania.

Ametaja vipaumbele vingine ni afya, elimu na maji.

Amesema ukatili wa kijinsia kwa watoto na vijana kwamba unakwenda kukomeshwa.