Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NFRA yafikia hifadhi ya tani laki nane za nafaka

Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Dk Andrew Komba.

Muktasari:

  • Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeendesha semina maalum kwa Maofisa Kilimo na Ugavi ili kuwajengea uwezo kuhusu mbinu bora za uvunaji na uhifadhi wa mazao baada ya mavuno (Post-Harvest Management).

Dodoma. Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza mafunzo maalum kwa Maofisa Kilimo na Ugavi wake nchini yakilenga kuboresha mbinu za uvunaji na uhifadhi wa mazao baada ya mavuno, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu wa ununuzi wa nafaka wa mwaka 2026/2027.

Akifungua semina hiyo inayofanyika katika Kituo cha Mtanana – Post Harvest Management Centre (PHMC) kuanzia Mei 24 hadi 26, 2026, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Dk Andrew Komba, aliwapongeza maafisa hao kwa mchango wao uliowezesha wakala kufikia hifadhi ya zaidi ya tani laki nane za nafaka katika mwaka 2024/2025, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa tangu kuanzishwa kwa NFRA.

Dk Komba alisema mafanikio hayo yametokana na usimamizi madhubuti wa majukumu ya msingi ya wakala ikiwemo ununuzi, uhifadhi, utoaji wa chakula wakati wa majanga pamoja na uuzaji na mzunguko wa chakula kwa lengo la kuhakikisha usalama wa chakula nchini.

Aidha, alibainisha kuwa Serikali inalenga kuongeza uwezo wa Taifa wa kuhifadhi chakula hadi tani milioni 3 ifikapo mwaka 2030, kwa mujibu wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Semina hiyo pia inalenga kuwajengea uelewa washiriki kuhusu matumizi ya mifumo ya kidigitali katika usimamizi wa ununuzi, pamoja na mbinu bora za kuhakikisha ubora wa nafaka na kupunguza upotevu baada ya mavuno.

Washiriki wanatarajiwa kutumia mafunzo hayo kuboresha utekelezaji wa majukumu yao kuelekea msimu ujao wa ununuzi wa nafaka 2026/2027.