Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Puma Energy yang'ara Tuzo ya Rais ya Mlipa Kodi Bora

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi (kulia), akimkabidhi Tuzo ya Rais ya Mlipa Kodi Bora katika kundi la Mwangizaji Bora wa bidhaa za vimiminika (Best Wet Cargo Importer) Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya nishati ya Puma Tanzania, Fatma Abdallah (kushoto), wakati wa hafla ya ugawaji wa tuzo iliyofanyika usiku wa leo Jumatano, Julai 1, 2026 ukumbi wa Mlimani City jijii Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Kampuni ya Puma Energy Tanzania imetunukiwa Tuzo ya Rais ya Mlipa Kodi Bora katika kipengele cha Muagizaji Bora wa Mizigo ya Vimiminika (Best Wet Cargo Importer), ikiwa ni kutambua mchango wake katika ulipaji wa kodi na uendeshaji wa biashara kwa kuzingatia sheria.

Tuzo hiyo ilitolewa katika hafla ya Tuzo za Rais kwa Walipa Kodi Bora iliyofanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambapo walipa kodi bora kutoka mikoa yote 35 ya Tanzania walitambuliwa kwa mchango wao katika kuongeza mapato ya Serikali.

Katika hafla hiyo, tuzo ya Puma Energy Tanzania ilikabidhiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah alisema kampuni hiyo inajivunia kutambuliwa kwa kuwa ni uthibitisho wa misingi yake ya uwajibikaji, uadilifu na uzingatiaji wa sheria katika uendeshaji wa biashara.

Alisema tuzo hiyo ni matokeo ya juhudi za wafanyakazi wa kampuni, ushirikiano mzuri na Serikali pamoja na dhamira ya kuendesha biashara kwa uwazi huku wakizingatia sheria za nchi.

"Tuzo hii ni heshima kubwa kwetu na inatupa nguvu ya kuendelea kutekeleza wajibu wetu kwa ufanisi. Tunaamini ulipaji wa kodi ni mchango muhimu katika kujenga uchumi imara na kuboresha huduma za kijamii kwa Watanzania," alisema Fatma.

Aliongeza kuwa kampuni itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuongeza mapato ya ndani kupitia ulipaji wa kodi kwa wakati, uwekezaji endelevu na upanuzi wa huduma za nishati zinazochochea ukuaji wa uchumi.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imechangia zaidi ya Sh1.4 trilioni kupitia kodi na tozo mbalimbali, jambo lililoifanya kuendelea kutambuliwa na TRA kutokana na utii wake wa sheria za kodi na mchango wake katika kuongeza mapato ya Serikali.

Mbali na ulipaji wa kodi, Puma Energy Tanzania imeendelea kuwekeza katika sekta ya nishati kupitia mtandao wa zaidi ya vituo 100 vya mafuta, kituo kikubwa cha kuhifadhi mafuta pamoja na maghala yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini.

Kampuni hiyo pia inasambaza mafuta ya ndege katika viwanja vinane vya ndege, ikiwemo viwanja vyote vya kimataifa nchini, huku ikiendeleza matumizi ya nishati safi kupitia Kituo Kikuu cha Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG Mother Station) na mtandao wa vituo vya CNG vinavyoendelea kupanuliwa katika mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro.

Aidha, imeendelea kupanua huduma za gesi safi ya kupikia kupitia Puma Gas pamoja na biashara ya vilainishi na maduka ya Shop Express, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma bora za nishati na kuchochea maendeleo ya uchumi wa Tanzania.