Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unyanyapaa dhidi ya waumini wa Shincheonji wazua mjadala UN

Dar es Salaam. Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Coordination des Associations et Particuliers pour la Liberté de Conscience (CAP LC) limewasilisha taarifa ya maandishi katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC), likieleza wasiwasi wake kuhusu kile linachodai kuwa ni kuongezeka kwa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya waumini wa Shincheonji Kanisa la Yesu katika baadhi ya nchi.

Taarifa hiyo iliwasilishwa wakati wa kikao cha 62 cha Baraza la Haki za Binadamu, ambapo CAP LC ilisisitiza kuwa maamuzi ya kiutawala na kimahakama yanayohusu makundi ya kidini yanapaswa kuzingatia ushahidi unaoweza kuthibitishwa na misingi ya sheria, badala ya taarifa ambazo hazijathibitishwa.

Kwa mujibu wa shirika hilo, mitazamo hasi inayodaiwa kuanzia Korea Kusini imeendelea kusambazwa katika mataifa mbalimbali, jambo ambalo linaweza kuathiri maoni ya umma na kuchangia maamuzi yanayowagusa waumini wa Shincheonji katika nyanja za utawala na sheria.

CAP LC ilionya kuwa endapo unyanyapaa dhidi ya kundi moja la kidini utaruhusiwa kuendelea bila kupingwa, hali hiyo inaweza kuweka katika hatari makundi mengine ya dini yaliyo wachache. Kutokana na hali hiyo, shirika hilo limezitaka serikali kuhakikisha kuwa haki ya uhuru wa kuabudu, usawa mbele ya sheria na ulinzi wa haki za binadamu vinazingatiwa kwa watu wote bila ubaguzi.

Kwa upande wake, Shincheonji Kanisa la Yesu limesema hatua ya CAP LC kuwasilisha suala hilo katika Baraza la Haki za Binadamu inaashiria kuwa mjadala kuhusu kanisa hilo sasa umevuka mipaka ya Korea Kusini na kuwa sehemu ya mjadala mpana wa kimataifa kuhusu uhuru wa dini na haki za binadamu.

CAP LC ni shirika lisilo la kiserikali lenye hadhi maalumu ya ushauri katika Baraza la Uchumi na Masuala ya Kijamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC). Kwa mujibu wa shirika hilo, limekuwa likiwasilisha katika Umoja wa Mataifa masuala yanayohusu uhuru wa dini na dhamiri pamoja na changamoto zinazolikabili makundi mbalimbali ya kidini duniani.

Katika taarifa yake, CAP LC pia ilitaja mifano kutoka Uingereza na baadhi ya nchi zinazozungumza Kijerumani, ikidai kuwa mitazamo hasi dhidi ya waumini wa Shincheonji imechangia ubaguzi wa kijamii, kuingiliwa kwa maisha binafsi na changamoto katika baadhi ya taratibu za kiutawala.

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa hupokea taarifa kutoka kwa mashirika yenye hadhi ya ushauri kama CAP LC, ambazo hutumika kuchangia mijadala kuhusu masuala mbalimbali ya haki za binadamu. Hata hivyo, kuwasilishwa kwa taarifa hizo hakuashirii kwamba Umoja wa Mataifa umeidhinisha au umekubaliana moja kwa moja na hoja zilizomo ndani yake.

Masuala ya uhuru wa dini, usawa mbele ya sheria na ulinzi wa haki za binadamu yanaendelea kuwa sehemu ya ajenda za Baraza hilo katika kujadili changamoto zinazozikabili jamii mbalimbali duniani.