Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wagombea udiwani CCM wawili walioongoza kura za maoni wakatwa Manyara

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Manyara, John Nzwalile akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa kura za maoni za udiwani Babati. Picha na Joseph Lyimo.

Muktasari:

  • Katika kata zote 142 za mkoa wa Manyara, wagombea udiwani wote wa CCM wamepitishwa ila kata mbili zilizopo kwenye wilaya za Simanjiro na Kiteto.

Babati. Wagombea udiwani walioongoza mchakato wa kura za maoni ya CCM katika kata 140 za Mkoa wa Manyara, wamepitishwa kugombea nafasi hizo isipokuwa kata mbili zilizopo kwenye Wilaya ya Simanjiro na Kiteto.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Manyara, John Nzwalile akizungumza na waandishi wa habari mjini Babati leo Jumamosi Agosti 16 mwaka 2025 amesema wagombea walioongoza kura za maoni kwa kata 140 wamepitishwa kasoro kata mbili.

Nzwalile amezitaja kata hizo mbili kuwa ni Loiborsiret iliyopo wilayani Simanjiro na kata ya Partimbo ya wilayani Kiteto.

Amesema mchakato wa kuhakikisha kata hizo mbili zinapata wagombea udiwani kupitia CCM unaendelea na watapatikana kwa siku mbili au tatu zijazo.

Ameeleza kwamba kuwa wa halmashauri kuu ya CCM ya mkoa huo, wamepitia mchakato wa shughuli za kura za maoni na kuwapitisha wagombea wa kata 140 na kasoro kata mbili.

"Walioongoza mchakato wa kura za maoni kwenye kata hizo 140 wameshaandikiwa barua za uteuzi ili waanze mchakato wakuchukua fomu za Tume," amesema Nzwalile.

Mmoja kati ya wanachama wa CCM wa kata ya Loiborsiret, Loishiye Mollel ameeleza kwamba wameshapata taarifa kuwa mchakato wa uchaguzi utafanyika Agosti 17 mwaka 2025.

Mollel amesema kuwa bado hawajaelezwa sababu ya kurudiwa kufanyika kwa uchaguzi huo ila wameshajiandaa kuhakikisha wao kama wajumbe wanashiriki kura hizo za maoni.

"Mchakato wa kura za maoni tutarudia tena kama tulivyoelezwa na viongozi wetu, hatuna budi kufanya hivyo na tumejiandaa kufanya hivyo," amesema Mollel.