Washindi watatu wa kampeni ya CRDB kuona kombe la dunia Canada
Meneja Mwandamizi wa Kadi wa Benki ya CRDB, Karington Chahe (kulia) akimkabidhi zawadi ya televisheni inchi 85 mshindi wa droo ya kwanza ya Fainali Ndo Mpango na TemboCard Visa, Theresia Mawalla.
Dar es Salaam. Mkuu wa mkoa wa Rukwa na mwanasiaka mkongwe nchini, Charles Makongoro Nyerere ni miongoni mwa wateja watatu wa Benki ya CRDB wamejishindia tiketi za kushuhudia moja kwa moja mechi ya fainali ya Kombe la Dunia nchini Canada kupitia kampeni ya Fainali Ndo Mpango na TemboCard Visa.
Washindi wengine ni Abdullauf Suleiman Muta na Arun Vithaldas Lodhia ambao wote wanatoka mkoa wa Dar es Salaam.
Washindi hao wanaungana na washindi wengine wa droo ya kwanza ambao ni Keneth Bina, Arnold Samugabo na Erick Mlinga, wote wakazi wa Dar es Salaam, pamoja na Gasper Melkiory Kavishe kutoka mkoa wa Morogoro.
Mbali na zawadi hiyo kubwa, wateja wengine watatu wamejinyakulia televisheni ya kisasa ya inchi 85, king’amuzi na kifurushi kitakachowawezesha kufuatilia mechi zote za fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Marekani, Mexico na Canada kuanzia Juni 11 hadi Julai 19.
Washindi wa zawadi hizo ni Amina Awadhi , Ester Kabakama, na Lusekelo Michael
Meneja Mwandamizi wa Kadi wa Benki ya CRDB, Karington Chahe (wa kwanza kulia) akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya pili ya Fainali Ndo Mpango na TemboCard Visa inayoendeshwa na benki ya CRDB. Wa pili kulia ni mfanyakazi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja wa CRDB PLC Tanzania Esther Mhagama na kushoto ni Queen Masanja ambaye ni Balozi wa chapa wa benki ya CRDB PLC .
Akizungumza kuhusu ushindi huo, Meneja Mwandamizi wa Kadi wa Benki ya CRDB, Karington Chahe, alisema washindi wamepatikana baada ya kutumia kadi za TemboCard Visa (Debit, Prepaid au Credit) kufanya malipo mbalimbali na hivyo kuingia moja kwa moja kwenye droo.
Aliwapongeza washindi hao na kuwahimiza wateja wengine kuendelea kutumia kadi hizo ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali.
Chahe aliongeza kuwa kampeni hiyo bado inaendelea, huku kukiwa na nafasi sita zaidi za kushinda safari ya Kombe la Dunia na saba za televisheni kubwa zenye vifurushi kamili vya kuangalia mechi zote.
Alisema lengo la kampeni hiyo ni kuwazawadia wateja na kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidijitali, akibainisha kuwa dunia inaelekea zaidi kwenye mifumo ya kidijitali, hivyo Watanzania wanapaswa kuendana na mabadiliko hayo.
“Kampeni hii ni sehemu ya jitihada za Benki ya CRDB kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidijitali, kuleta ubunifu katika huduma za kifedha na kuwazawadia wateja wetu kwa uaminifu wao,” alisema.
Alifafanua kuwa mteja anayefanya angalau miamala 30 kwa mwezi kupitia TemboCard Visa kwenye mashine za POS au mtandaoni huingia moja kwa moja kwenye droo ya kushinda.
Meneja Mwandamizi wa Kadi wa Benki ya CRDB, Karington Chahe (wa kwanza kulia) akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya pili ya Fainali Ndo Mpango na TemboCard Visa inayoendeshwa na benki ya CRDB. Wa pili kulia ni mfanyakazi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja wa CRDB PLC Tanzania Esther Mhagama na kushoto ni Queen Masanja ambaye ni Balozi wa chapa wa benki ya CRDB PLC .
Wakati huo huo, washindi wawili wa droo ya kwanza kwa upande wa zawadi ya televisheni wamepatiwa zawadi zao.
Washindi hao ni Samson Mkumbo na Theresia Mawalla ambao wote ni wakazi wa Dar es Salaam. Mshindi mwingine Eunice Masigati wa Dodoma alipokea zawadi yako huko huko Dodoma.
Washindi hao walikabidhiwa zawadi zao na meneja wa migogoro na ufuatiliaji wa Miamala ya Kadi wa benki ya CRDB PLC Tanzania, DR Congo na Burundi, Flora Josephat Mackanja na Chahe.