Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvua yasitisha ujenzi wa barabara Zanzibar

Msongamano wa magari uliosabaishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo ya Round about Kwerekwe mjini Unguja. Picha na Muhammed Khamis

Muktasari:

  • Mvua kubwa ilioanza kunyesha alfajiri ya kuamkia leo imesitisha kwa muda ujenzi wa barabara mpya zinazoendelea maeneo mbali mbali ya kisiwani humo.

Unguja. Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Zanzibar zimesababisha usitishwaji kwa muda ujenzi wa barabara zinazondelea kujengwa maeneo mbali mbali ya Unguja.

Mvua hiyo ilianza majira ya saa kumi na mbili asubuhi leo Novemba Mosi, 2023 katika maeneo tofauti, licha ya kuwa hadi sasa bado hakuna taarifa yoyote ile ya madhara.

Mwananchi Digital imeshuhudia kukikosekana harakati zilizoeleka za ujenzi wa barabara katika maeneo ya Mombasa pamoja na Mtoni.

Pia kumekua na foleni kubwa ilioyosababishwa na mvua hiyo kwa kuweka msomgamano wa magari huku ikiwalazimu madereva kutumia zaidi ya saa moja barabarani sehemu ya mwendo wa dakika 15.

Wakati hayo yakijiri shuguli mbalimbali za kijamii zimekumbwa na changamoto ikiwemo utolewaji wa huduma za bidhaa katika Soko la Mwanakwerekwe.

Baadhi ya wanachi visiwani hapa wameiambia Mwananchi Digital kuna haja ka kuweka mazingira rafiki hususani kwenye maeneo ya masoko.

Salum Abdallah ameiambia amesema kuwa kupindi hiki ambacho Serikali inajenga upya masoko mengi kuna haja ya Baraza la manispaa kufanyia ukarabati haraka sana walau kuweka kifusi kwenye Soko la Kwerekwe.

"Soko lile ndio linalotegemewa na wengi lakini katika kipindi hichi cha mvua nina hakika hakutakwendeka kabisa maana mazingira yake sio rafiki," amesema.