Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwinyi amteua Shariff kuwa mjumbe Baraza la Wawakilishi

Shariff Ali Shariff mjumbe wa baraza la wawakilishi.

Muktasari:

  • Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamesema huenda Shariff ameteuliwa ili awe Waziri wa Nchi, Ofisi Rais, Kazi Uchumi na uwekezaji, wizara ambayo haina waziri mpaka sasa.

Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amemteua Shariff Ali Shariff kuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi.

Uteuzi huo ni kwa mujibu wa uwezo aliopewa Rais chini ya kifungu namba 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Shariff ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (Zipa).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, Februari 13, 2024 kwa vyombo vya habari na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu kiongozi, Zena Said.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamesema huenda Shariff ameteuliwa ili awe Waziri wa Nchi, Ofisi Rais, Kazi Uchumi na uwekezaji, wizara ambayo haina waziri mpaka sasa.

Awali, wizara hiyo ilikuwa ikiongozwa na Mudrick Ramadhan Soraga, ambaye Januari 26, 2024 Rais Mwinyi alimteua kuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale baada ya aliyekuwa ameshikilia nafasi hiyo, Simai Muhamed Said kujiuzulu.

Akizungumza na Mwananchi Digital, mchambuzi wa masuala ya siasa kisiwani hapa, Saleh Said amesema kwa mazingira yalivyo inawezekana Shariff kuna uwezekano mkubwa wa kuteuliwa kushika wadhifa huo.

Salehe amesema Shariff kwa kipindi ambacho ameongoza taasisi hiyo ambayo ipo chini ya Wizara ya Uwekezaji, kumekuwa na mafanikio ya waziwazi na kukuza uwekezaji kisiwani hapo.


Alama za Shariff akiwa Zipa

Mamlaka hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2020 hadi Novemba 30, 2023 Zipa ilisajili miradi 296 yenye mtaji wa Dola bilioni 4.5 za Marekani (Sh11.3 trilioni)

Miradi hiyo inatarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 17,479 kati ya hiyo inayohusisha uwekezaji katika sekta ya hoteli ni 112, biashara ya majengo 56, viwanda 36 na mingine ni ya sekta nyinginezo.

Katika kipindi chake Shariff, visiwa vidogo 16 kati ya 20 vimewekezwa vikiwa na thamani ya Dola milioni 384.5 za Marekani (zaidi ya Sh970 bilioni).