Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Mwinyi ateua 25, wamo majaji wa Mahakama Kuu

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi

Muktasari:

  • Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewateua viongozi 25 kushika nyadhifa mabalimbali visiwani humo kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Baraza la Mapinduzi, Zena Said, iliyotolewa leo Alhamisi Novemba 9, 2023.

Dar es Salaam. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewateua viongozi 25 kushika nyadhifa mabalimbali visiwani humo wakiwemo Majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Uteuzi huo uliotangazwa leo jioni, Novemba 9, 2023 na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Said ambapo imewataja Khadija Shamte Mzee, ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Zanzibar ambapo awali alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar.

Pia, amemteua Haji Suleiman Khamis (Tetere) kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Zanzibar. Kabla ya Uteuzi Ndugu Haji alikuwa Wakili wa Kujitegemea.

Aidha, uteuzi huo pia umemgusa Salum Hassan Bakari ambaye sasa atakuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Kabla ya uteuzi Salum alikuwa Naibu Mrajis wa Mahakama Kuu.

Viongozi wengine walioteuliwa ni Sheha Makame Mussa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar. Sheha ni mstaafu wa utumishi wa umma.

Pia, Dk Mahmoud Abdulwahab Alawi, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Sheria la Mawasiliano Zanzibar (ZICTIA). Dk Alawi ni Mkuu wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar.

Rais Mwinyi amemteua Balozi Omar Yussuf Mzee amemteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS). Balozi Omar ni waziri mstaafu wa awamu ya saba.

Mohamed Aboud Mohamed, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Udhibiti wa Leseni za Biashara (BLRC). Mohamed ni waziri mstaafu awamu ya saba.

Kidawa Hamid Saleh ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC). Kidawa ni mstaafu wa awamu ya saba.

Katika uteuzi huo, Rais Mwinyi amemteua Akif Ali Khamis kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mwani Zanzibar. Akif ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar.

Jamila Shaaban Salum, ameteuliwa kuwa Mkurugenznzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Biashara na Macndeleo ya Viwanda. Jamila alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Sera wa Ofisi ya Rais, Tawala Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maaluum.

Pia, Rais Mwinyi amemteua Abdul-latif Khatib Haji kuwa Mkurugcnzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Afya. Kabla uteuzi huo Abdul-latif alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Kugharamia Huduma za Afya.

Bihindi Nassor Khatib ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji. Khatib alikuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Uteuzi huo umemhusu Mohamed Hassan Khamis aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini. Mohamed alikuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Nana Rowland Mwanjisi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa  Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango. Nana alikuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Makaazi.

Mhaza Gharib Juma ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi. Mhaza alikuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

Ilyasa Pakacha Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais. Haji aliwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi.

Daima Mohamed Mkalimoto ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Daima alikuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.

Hannat Bakar Hamad ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa dara ya Maendeleo ya Makaazi Zanzibar katika Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi. Hannat alikuwa Afisa Sheria Shirika la Bandari Zanzibar.

Haji All Haji ameteuliwa Kamishana wa Sera za Kodi na Fedha katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango. Haji alikuwa Mkurugenzi Idara ya Sera za Kodi na Fedha Zanzibar.

Mwanaidi Ramadhan Juma ameteuliwa kuwa Kamishna wa Usimamizi wa Sera za Ununuzi wa Umma wa Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango. Mwanaidi alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi wa Umma wa Wizara ya Maendeleo ya Jinsia, Wazee na Watoto.

Zena Mahmoud Hassan ameteuliwa kuwa Kamishna wa Bajeti wa Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango. Zena alikuwa Afisa Mwandamizi wa Idara ya Bajeti.

Mohamed Fakih Mzee ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Huduma Sheria katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango. Awali alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Khamis Juma Khamis ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Udhibiti wa Leseni za Biashara (BLRC). Khamis alikuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Ardhi.

Akif All Khamis ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar. Akif alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zannibar.

Dk Abdul-Nasser Rashid Hikmany ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Ardhi Zanzibar. Alikuwa Mrajis wa Ardhi.