Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Mwinyi akabidhiwa ramani ujenzi mji mpya Zanzibar

Jinsi Mji huo utakavyokuwa

Muktasari:

  • Awali mradi huu ulipangwa kujengwa eneo la Kilimani Wilaya ya Mjini, lakini wananchi wa eneo hilo walishindwa kukubaliana huku ikitajwa kuingiliwa na masuala ya kisiasa, sasa Serikali imetafuta eneo jingine nje ya mji.

Unguja. Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi amekabidhiwa mfano wa ramani ya mji mpya wa biashara, Nyamanzi Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amekabidhiwa ramani hiyo leo Ijumaa, Desemba 15, 2023 Ikulu Zanzibar na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban, huku akipongeza hatua za awali zilizofikiwa na wazo la ujenzi wa mji huo.

“Hii ni hatua nzuri, hongereni kwa ubunifu huu kutaka kujenga mji mpya wa biashara,” amesema Rais Mwinyi.

Kwa upande wake, Waziri Shaabani amemweleza Rais Mwinyi hatua za awali za mpangokazi wa ujenzi wa mji huo mpya wa kisasa zimekamilika, baada ya kukaa pamoja na kampuni ya HEERIM ya Korea ya Kusini inayotarajiwa kupewa zabuni ya ujenzi wa mji huo.

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Said Shaaban akimkabidhi Rais Hussein Mwinyi mfano wa ramani ya ujenzi wa Mji mpya wa biashara Nyamanzi.

Amesema mji mpya wa Nyamazi ni mmoja ya miradi mikubwa ya kimkakati, utarajiwa kuwa na awamu nne za maendeleo ya biashara na uwekezaji.

Awamu ya kwanza ya matarajio ya ujenzi huo ni ujenzi wa ukumbi mkubwa wa kisasa wa mikutano ya kimataifa unaotarajiwa kuchukua idadi kubwa ya watu pamoja na kuhusisha vivutio vya wageni watakaotembelea eneo hilo vitakavyopamba haiba ya ukumbi.

Awamu ya pili ya ujenzi wa mji huo utahusisha hoteli kubwa za kisasa zenye hadhi ya nyota tano na awamu ya tatu ni ujenzi wa eneo la kisasa la biashara litakalohusisha maduka makubwa na vivutio vingine vya biashara na utalii.

Waziri Shaaban ametaja awamu ya nne ya ujenzi wa mji huo ni eneo la makazi ya wananchi yakayohusisha mji mpya uliopangika kwa ustadi na haiba itakayovutia mandhari ya eneo husika.

Kama hayo hayatoshi, mji huo utahusisha ujenzi wa hospitali kubwa ya kisasa pamoja na kuwekwa viwanja vya michezo vitakavyokidhi haja ya wakazi wa eneo hilo na wageni wengine watakaoutembelea.