Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Mwinyi akaribisha wawekezaji vyuo vikuu vya kimataifa

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Elimu ya Juu na Teknolojia Afrika( QS AFRICA FORUM 2025).

Muktasari:

  • Mpango huo unaangazia ushirikiano baina ya tasisi za utafiti, ubunifu na elimu ya juu ili kuziunganisha pamoja kuleta mapinduzi kielimu.

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar inaweza kutengeneza nafasi kubwa ya kuwa kituo cha elimu ya ubunifu kikanda na kimataifa kutokana na hatua kubwa iliyopiga ya kimaendeleo katika sekta ya elimu.

Amesema, Serikali itaendelea kutumika kama daraja kati ya Afrika na dunia, na kati ya ujuzi na fursa kutokana na usalama na amani iliyopo hivyo katika kulitambua hilo ndio maana imefungua milango yake kuvikaribisha vyuo vikuu kuwekeza kisiwani hapo.

Rais Mwinyi ameyasema hayo leo Jumatatu Julai 3, 2025 wakati akifungua Mkutano wa Elimu ya Juu na Teknolojia Afrika (QS Africa Forum 2025).

"Milango yetu iko wazi kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza vyuo vya kimataifa kisiwani hapa, ambapo kwa sasa tuna chuo kikubwa cha kimataifa cha IIT Madras, kupitia hilo linaweza kuifanya Zanzibar kuwa kituo cha ubunifu na utafiti katika masuala ya elimu ya juu," anasema Dk Mwinyi. 

Pia, amesema anatambua kazi kubwa inayofanywa na Taasisi ya QS kwakuaendelea kutekeleza sio tu katika kuinua ubora wa kitaaluma duniani kote, lakini katika kuunda ajenda ya elimu ya juu duniani katika enzi ambazo maarifa ni muhimu kwa maendeleo kwani mfumo wa QS hujenga madaraja kati ya mabara.

Ameeleza kuwa jambo muhimu ni kuwa na ushirikiano na vyuo vikuu pamoja na taasisi za elimu ya juu barani Afrika na duniani, ili kutoa fursa ya kuunganishwa kwa vyuo kwa ajili ya kufanya tafiti, ubunifu na matumizi ya teknolojia ili kuimarisha elimu ya juu.

Rais Mwinyi ameeeleza kuwa kwa sasa ni wakati wa kuonesha kwa vitendo uwajibikaji wao kwani fursa ipo mbele yao ni vyema kuitumia.

Amewataka, wote waliohudhuria katika mkutano huo kuamsha fikra na mawazo yao kwa kujenga ushirikiano ambao utaleta siyo tu maendeleo ya Afrika, bali maendeleo ya wanadamu wote.

Hivyo, amesema Serikali ya Zanzibar itaendelea kutumika kama daraja kati ya Afrika na dunia, na kati ya ujuzi na fursa hivyo ameomba mkutano huo ukumbukwe kama hatua ya kusonga mbele, ambapo sauti za kiafrika zilikusanyika ili kuendeleza mafunzo, uvumbuzi, na ushirikiano wa maana kwa mustakabali wa pamoja.

Akizungumzia suala la teknolojia ya akili mnemba (AI), Dk Mwinyi amesema kuwa Zanzibar haipaswi kubaki nyuma katika matumizi ya teknolojia hiyo, lakini ni lazima ihakikishe kuwa inapata manufaa na faida zake, sambamba na kuhakikisha udhibiti wa athari zake kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa za kielimu.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Chuo cha Morden College of Business and Science nchini Oman (MCBS), Dk Munneer AL Maskari katika Mkutano wa Elimu ya Juu na Teknolojia Afrika( QS AFRICA FORUM 2025).

Naye, Mwenyekiti Mtendaji wa Chuo cha Morden College of Business and Science nchini Oman (MCBS), Dk Munneer AL Maskari amesema mkutano huo unaangazia ushirikiano baina ya tasisi za utafiti, ubunifu na elimu ya juu ili kuziunganisha pamoja kuleta mapinduzi kielimu.

Pia, amesema mkutano huo unalenga kuviunganisha vyuo vikuu vya vya Afrika katika kukuza elimu ya juu, teknolojia na ubunifu ili kufanya tafiti katika masuala mbalimbali ikiwemo miundombinu ya elimu.

Amesema, wanampango wa kuisaidia Zanzibar kufanya tafiti zake ambapo kwa sasa wameanza kufanya baina ya chuo hicho na IIT Madras wakiwa na lengo ya kuiweka Zanzibar katika ramani ya kimataifa kwa masuala ya elimu na utalii.

Ofisa Mkuu wa Biashara kutoka  Taasisi ya QS, Jason Newman amesema huu ni wakati wa elimu ya Afrika kuwekwa katika uso wa dunia ili kuendana na kasi ya mabadiliko na kupata fursa ya kutengeneza maisha yao kupitia ujuzi wanaojifunza.

Amesema, Zanzibar imekuwa ni miongoni mwa nchi inayotoa elimu kimataifa kupitia chuo IIT Madras hivyo ni sifa mojawapo kuionesha dunia juu ya ufanyaji kazi wake na hiyo itakuwa fursa kubwa kwa vyuo vyengine kuwekeza hapo.

Pia, amesema taasisi hiyo ina mikakati madhubuti wa kufanya kati na vyuo vya Serikali na binafsi ili kuifikia jamii moja kwa moja na kubadilisha mitazamo yao juu ya elimu kwani kila mmoja anahitaji kufika mbali zaidi ya alipo.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohammed Mussa amesema mkutano huo umekuja kutoa fursa kwa Tanzania kuwekeza katika vyuo vikubwa kwa kuwa na ushirikiano mkubwa ili kufanya tafiti zinazokidhi mahitaji.