Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zanzibar kushughulikia changamoto za wanamichezo wanawake

Dar es Salaam. Wakati Ligi ya Wanawake Zanzibar ikitarajia kuanza, Serikali imesema imefanyia kazi changamoto mbalimbali zinazokwamisha ushiriki wao katika michezo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Tabia Maulid Mwita wakati akizungumza katika mahojiano maalumu kabla ya kufanyika kwa kongamano la miaka mitatu ya Rais Dk Hussein Ali Mwinyi madarakani.

Tabia amesema ili kuongeza ari ya wanawake katika michezo, wanaendelea kusimamia vilabu na kutatua changamoto zinazowafanya wanawake washindwe kujitokeza kwa wingi kushiriki.

"Tunaendelea kushirikiana na sekta nyingine kama Wizara ya Elimu ili waweze kutoa elimu ya umuhimu wa michezo kwa wanawake, kuwasaidia wanawake kukabiliana na hedhi kwa sababu ni changamoto inayowafanya wanawake kurudi nyuma kuingia kwenye changamoto za michezo," amesema Tania.

Amesema pia wamekuwa wakishikiriakiana na taasisi mbalimbali ili kuwajenga wanawake kuwa wanaweza kushiriki katika michezo.

"Hivyo ligi ya wanawake msimu huu itakuwa ni ligi nzuri kwani tutakuwa tumefanya maboresho mambo mengi na kuongeza timu za wanawake kwa upande wa Unguja na Pemba kwani tumekaa na chama cha michezo na kupeana mikakati mbalimbali ili kuhakikisha wanaweza kuendeleza vilabu vya wanawake," amesema Tabia.

Amesema vilabu vya wanawake vipo vingi lakini vilikuwa havina usajili jambo ambalo linafanyika sasa ili kupata takwimu sahihi.

Katika hilo pia wamekuwa na wamekuwa na mafunzo ya michezo ya wanawake viongozi wanawake katika michezo ikiwemo vile vya mpira wa miguu.

Katika habari, Tabia amesema kipindi cha miaka mitatu wametekeleza masuala mbalimbali yanayohusu uboreshaji na utoaji wa habari.

"Kwenye utamaduni tumehakikisha tunaimarisha utamaduni wa Mzanzibari katika kuulinda na kuutetea. Kwenye michezo tumejenga na kuvifanyia maboresho viwanja vya michezo na kuwaandaa wachezaji kushiriki mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Waziri wa Ujenzi na Miundombinu, Dk Khalid Salum  Mohamed amesema hali ya utengenezaji wa miundombinu ya barabara imefanyika ipasavyo na maeneo yote mijini na vijiji kazi ya ujenzi inaendelea.

"Kila jimbo siyo chini ya barabara mbili zinajengwa. Kwa hapa mjini kilomita 100.9 za barabara zinajengwa na kwa upande wa vijijini kilomita 275.9 zinaendelea kujengwa," amesema.

"Kwa barabara za mijini ujenzi umefikia asilimia 24 wakati barabara za vijijini tumefikia asilimia 25. Tunampongeza Rais Dk Mwinyi kwa kuwa kazi inayofanyika katika eneo la miundombinu haijawahi kufanyika," amesema Mohamed.

Katika upande wa viwanja vya ndege, amesema hivi karibuni wanataka kuanza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba ambao utakuwa wa kimataifa.

"Jana tumesaini mkataba wa kujenga jengo lingine la abiria katika Uwanja wa Abeid Aman Karume," amesema Mohamed.