Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akisoma barua ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoelezea kutohusika na taarifa zilizovuja kuhusu ripoti ya ukuaji wa uchumi wa nchi, alipokuwa akimpa taarifa Mbunge wa Momba (Chadema), David Silinde aliyesema ripoti hiyo haikujumuisha ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea kujengwa nchini, wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/2020 bungeni jijini Dodoma leo. Picha na Ericky Boniphace