Serikali yaagiza mbolea nje ya nchi kukabiliana na upungufu Kufuatia upungufu wa mbolea uliosababisha kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo, Serikali imesema imeagiza nje ya nchi ili kukidhi mahitaji yaliyopo.
Jela miaka 30 kwa kubaka, unyang’anyi Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemhukumu Selemani Nyigo miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi na kumbaka raia wa Ujerumani ambaye alikuwa mwalimu wa kujitolea Shule ya Sekondari Cagliero.
Watu wasiojulikana wadaiwa kumbaka mwanamke hadi kufa Iringa Watu wasiojulikana wamedaiwa kumbaka mwanamke mmoja hadi kufariki dunia na mwili wake kukutwa kwenye shimo la taka (dampo) katika Mtaa wa Mtwivila C uliopo Manispaa ya Iringa.
Watu 19,898 wapata chanjo ya Uviko-19 Iringa MKuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga amesema hadi kufikia Oktoba 14, 2021 Mkoa wa Iringa ulikuwa na jumla ya watu 19,898 waliochanjwa chanjo ya Uviko-19 aina ya Johnson.
Wazazi, walezi wasiotoa ushahidi wa ubakaji kukamatwa Serikali Mkoani Iringa imesema itawakamata wazazi na wanafamilia wanaoshindwa kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya vitendo vya ubakaji na ulawiti walivyofanyiwa watoto.
RC Sendiga atangaza vita Iringa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amesema mwananchi atakayekamatwa na mafuta yanayotumika katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Nduli atafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi...
Wajawazito wahimizwa kupata chanjo Uviko 19 Mganga mkuu wa manispaa ya Iringa, Dk Jesca Lebba amewataka wajawazito na wanaonyonyesha kupata chanjo ya Uviko-19 ili kuimarisha kinga za mwili za mama na mtoto.
Jaji Mkuu aiomba Serikali kuongeza magereza kila wilaya Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma ameiomba Serikali kuongeza ujenzi wa magereza kwa kila wilaya ili kupunguza misongamano ya mahabusu na ucheleweshaji wa kesi.
Kibano kipya viongozi wa mikoa Wakuu wa mikoa na wilaya nchini wanakabiliwa na kibano kingine cha Rais Samia Suluhu Hassan cha kuhakikisha kwamba asilimia 40 ya mapato ya halmashauri zinakwenda kwenye miradi ya maendeleo...
Anayetuhumiwa kumuua mpenzi wake Iringa kortini Aliyekuwa Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa (Tumaini), fani ya uandishi wa habari mwaka wa pili, Prudence Patrick (21) amefikishwa kakika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa akituhumiwa kumuua...