Afungwa maisha gerezani kwa kumbaka mtoto wa miaka sita
Mkazi wa Ilembo, Kata ya Vwawa wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe, Betwel Anyalwisye (51), amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka sita.