Atupwa jela miaka 30 kwa kumbaka mtoto wa miaka 13 Rombo
Mahakama ya Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, mkazi wa Kijiji cha Mbomai, wilayani humo, Ally Mbwambo (41) kwa kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 13.