Dk Magufuli Rais mteule

Thursday October 29 2015

 

By Claud Mshana

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemtangaza Dk John Magufuli kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili ya Oktoba 25, mwaka huu.

Dk Magufuli ameshinda kwa jumla ya kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46 ya kura zote.

Katika uchaguzi huo, mgombea wa Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa amepata kura 6,072,848 ambazo ni sawa na asilimia 39.97 ya kura zote halali.

Mgombea wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira amekuwa wa tatu kwa kupata kura 98,763