Alichokisema Sallam kuhusu Diamond

Saturday April 04 2020
pic samal

Dar es Salaam. Kama ni mfuatiliaji wa burudani hakika utakuwa umekumbana na mjadala kuhusu kuhusu Sallam SK ambaye ni meneja wa Diamond Platnumz  kuacha kumsimamia mkali huyo wa wimbo wa Jeje.

Mjadala huo ulitokana na Sallam kubadili baadhi ya taarifa zake katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

Awali, aliandika kuwa ni meneja wa Diamond  huku akitaka watu wanaotaka kuwasiliana na msanii huyo waanzie kwake.

Jana Ijumaa Aprili 3, 2020, Sallam alibadili maelezo hayo na kujitambulisha kuwa ni mfanyabiashara, jambo lililoibua mjadala mitandaoni huku baadhi ya wachangiaji wakidai huenda amejiengua katika lebo ya Wasafi.

Leo Jumamosi Aprili 4, 2020 katika ukurasa huo, Sallam ameweka picha akiwa na Diamond na  kuandika, “umewaona wale wanataka kuboost viblog vyao vimekosa habari. Sasa wacha tuwape habari njema au unasemaje Diamond, wajiandae leo au kesho.”

Diamond naye alijibu ujumbe huo kwa kuandika, “nakusikiliza mzee Prodesa, wee nipe su, nisusushe.”

Advertisement

Mmoja wa mameneja wa msanii huyo,  Babu Tale  ameandika, “Menedez sema muda tupasue jipu.”

Baadhi ya watu waliotoa maoni yao kuhusu ujumbe huo akiwemo Sells Beats amesema "achia ngoma mpya watu wapo lock down, wanatakiwa wakatazame video nzuri YouTube.”

 

IQ Msafi, amesema “mtakoma mliojifanya  mnatusimulia ya Sallam na Diamond.”

Advertisement