BURUDANI: Wema Sepetu afunguka alivyotoa mimba mbili za Kanumba, akata tamaa kupata mtoto

Wednesday February 5 2020

 

By Thomas Matiko

Nairobi, Kenya .MWIGIZAJI maarufu wa Bongo Wema Sepetu sasa kama vile kakata tamaa ya kupata mtoto baada ya kudai anaamini anaandamwa na lawama ya kutoa mimba mbili.

Akifunguka kupitia Wema App, mwigizaji huyo ambaye katoka kimapenzi na takriban kila staa wa showbiz kule Bongo, alifichua alitoa mimba mbili za mwigizaji marehemu Steven Kanumba.

Wema kafichua ujauzito wa kwanza alioutoa ulikuwa ni makubaliano kati yake na Kanumba lakini aliponasa ya pili, aliitoa kimyakimya pasi na mwenzake huyo kujua. Uamuzi wa kutoa mimba hizi anasema ulichangiwa na sababu alijiona alikuwa bado ni mdogo sana na alikuwa angali ana muda wa kuja kupata mtoto baadaye, lakini hiyo imebaki kuwa stori.

Walipoachana, Wema anasema Kanumba alimtamkia hatawahi kupata mtoto na mwanamume yeyote kwa sababu ya kitendo hicho cha kutoa mimba zake.

Kauli hiyo Wema anaamini iligeuka na kuwa laana na ndio sababu hata baada ya kung’ang’ana mara zaidi ya elfu kwa miaka kadhaa iliyopita, hajaweza kufanikiwa huku kwa sasa akiwa tayari ananukia umri wa miaka 32.

Wema anasema ameshaikubali hali hiyo ya kuwa huenda asiwahi kuwa mama, akishikilia kuwa anajutia sana maamuzi aliyoyafanya hapo mwanzoni ila hamna jinsi ila kuvumilia sasa.

Advertisement

Advertisement