Yondo sister awakumbuka mashabiki Tanzania, Kenya baada ya miaka 24

Friday August 30 2019

 

By Faraji Issah, Mwananchi

Dar es salaam. Mwanamuziki na mnenguaji nguli mwenye asili ya Kongo Yondo Sister kutumbuiza nchini Kenya na Tanzania.

Akizungumza na gazeti la Daily Nation jijini Nairobi Kenya, amesema licha ya kuwa hakupanga kufanya shoo katika nchi hizo kwa sababu yupo likizo nchini Kenya, itamlazimu kufanya shoo Kenya na Tanzania ili kuungana na mashabiki zake wapya na wa zamani.  

Takribani  miaka 24 tangu  mwanamuziki huyo alipotembelea  nchini humo  alisema baada ya kuwasili jijini Nairobi siku ya Jumatano anatamani kuonana na mashabiki zake wa zamani.

Mashabiki wa mwanamama huyo anayetamba na miondoko ya bolingo wa nchini Kenya watapata nafasi ya kumuona katika uzinduzi wa Tembo hoteli  siku ya Ijumaa atakapo kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo la uzinduzi.

“Ingawa sikupanga kufanya onyesho lolote nikiwa likizo bado naangalia uwezekano wa kufanya shoo katika nchi hizi mbili, ”amesema.

Katika uzinduzi wa hoteli hiyo, Yondo Sister atasindikizwa na wasanii wa bendi za muziki wa Kikongo nchini Kenya ikiwamo Mangelepa inayoongozwa na mwimbaji na mtunzi mkongwe Kabila Kabanze “Evan.”

Advertisement


Advertisement