Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NEC yatoa orodha ya vyama uchaguzi wa madiwani

Muktasari:

  • NEC imesema wagombea 30 waliwekewa pingamizi na wenzao na Msajili wa Vyama vya Siasa kutokana na sababu mbalimbali.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema vyama 13 vimesimamisha wagombea katika uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26,2017.

Taarifa ya NEC iliyotolewa leo Jumanne Oktoba 31,2017 imevitaja vyama hivyo na idadi ya kata kwa kila chama kama ifuatavyo: ACT -Wazalendo wagombea 18 (sawa na asilimia 40), ADA-Tadea (1 - asilimia 2), ADC (4 - asilimia 7), CCM (43- asilimia 100), Chadema (42 - asilimia 98), Chauma (1 - asilimia 2) na CUF (30 - asilimia 70).

Vyama vingine ni DP (3 - asilimia 5), NCCR-Mageuzi (6 - asilimia 16), NRA (2 - asilimia 5), SAU (2 - asilimia 5), TLP  (1 - asilimia 2) na UDP (2 - asilimia 5).

NEC imesema Oktoba 26,2017 ilifanya uteuzi wa wagombea kwa ajili ya uchaguzi mdogo katika kata 43 zilizopo kwenye halmashauri 36 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika Novemba 26,2017.

Imesema wagombea 177 wa vyama mbalimbali walichukua fomu za uteuzi na za maadili ya uchaguzi.

Taarifa imesema, kati yao 174 sawa na asilimia 92.7 ni wanaume na 13 sawa na asilimia 7.3 ni wanawake.

“Wagombea 155 sawa na asilimia 87.6 ya waliochukua fomu za uteuzi walizirejesha na kuteuliwa kuwa wagombea,” amesema.

NEC imesema kati yao 145 sawa na asilimia 93.6 ni wanaume na wagombea 10 sawa na asilimia 6.4 ni wanawake.

Tume imesema hadi muda wa mwisho wa uteuzi ulipofika saa 10:00 jioni, wagombea 22 sawa na asilimia 12.4 ya waliochukua fomu hawakuteuliwa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kutorudisha fomu, kurudisha fomu nje ya muda uliotakiwa kisheria na fomu kutojazwa ipasavyo.

NEC imesema wagombea 30 sawa na asilimia 19.4 ya walioteuliwa waliwekewa pingamizi na wenzao na Msajili wa Vyama vya Siasa kutokana na sababu mbalimbali.

Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi, kampeni zimeanza na zitaendelea hadi Novemba 25,2017 ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi.