Mahakama yawatia hatiani Sugu, Masonga

Muktasari:
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite aliyeanza kusoma hukumu leo Februari 26,2018 saa 03:32 asubuhi amesema washtakiwa wana hatia kwa makosa waliyoshtakiwa.
Mbeya. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imewatia hatiani mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite aliyeanza kusoma hukumu leo Februari 26,2018 saa 03:32 asubuhi amesema washtakiwa wana hatia kwa makosa waliyoshtakiwa.
Baada ya kuwatia hatiani washtakiwa, hakimu Mteite anasubiriwa kutamka adhabu dhidi yao.
Sugu na Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
SOMA ZAIDI- Hukumu kesi ya Sugu, Masonga inasomwa