Baba, binti wa miaka minane washikiliwa tuhuma za mauaji

Thursday July 25 2019

 

By Hamida Shariff, Mwananchi [email protected]

Morogoro. Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia baba na mtoto wake wa miaka minane kwa tuhuma za kumuua mtoto wa jirani yao mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba kwa kumkata mapanga kichwani.

Tukio hilo lilitokea Jumapili Julai 21, 2019 saa nane mchana katika Kijiji cha Hembeti wilayani Mvomero mkoani Morogoro na mwili wa mtoto huyo, Greyson Valentino ulikutwa umefichwa kwenye shamba la watuhumiwa ukiwa na majeraha.

Akizungumzia tukio hilo jana Jumatano Julai 24, 2019, kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa aliwataja watumiwa hao kuwa ni Said Stephen ambaye ni baba na mwanaye wa kike (jina linahifadhiwa), mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Mpapa, Wilaya ya Mvomero.

Kamanda huyo alisema siku ya tukio baba wa marehemu, Simon Shedrack akiwa kanisani alipata taarifa kuwa mtoto wake amepotea na hivyo aliamua kurudi nyumbani kuanza kumtafuta kwa kushirikiana na majirani zake.

Soma gazeti la Mwananchi la leo Alhamisi Julai 25, 2019 kwa taarifa zaidi

Advertisement