Diamond amfagilia Hamisa Mabetto ila Zari mh!

Muktasari:

Diamond amebalikiwa kupata watoto wawili na Zari huku akiwa na mtoto mmoja na Hamisa Mobetto.

Dar es Salaam. Mwanamuziki Diamond Platnumz amesema Hamisa Mobetto ni muelewa katika suala la mawasiliano ya mtoto wake kulinganisha Zari.

Diamond alisema Hamisa amekuwa muelewa ninapohitaji kuwa karibu na mtoto wake tofauti na Zari amekuwa mgumu tangu baada ya kuachana.

"Unajua mimi sio kwamba sipendi kuwasiliana na wanangu ila sema Zari ametumia fimbo ya kunichapa kupitia watoto, yaani hasira za kuachana mimi na yeye amezihamishia kwa watoto ndio maana amebiblock ili nisipate nawasiliano nao, lakini najua hii ni hasira na itaisha tu.

"Kwa sasa nimebaki na mawasiliano na mtoto wangu wa hapa Tanzania niliyezaa na Hamisa na nashukuru Hamisa kwenye hili amekuwa ni muelewa sana," alisema Diamond