Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LHRC yaeleza mipango yake ya miaka sita ijayo

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga kushoto akizungumza na wanahabari kuhusu ushirikiano wa na Sweden  kulia ni Balozi wa nchi hiyo  Andres Sjoberg.

Muktasari:

  • Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimezindua mpango kazi wa miaka sita huku kikibainisha mikakati yake yenye lengo la kuboresha na kubadilisha sheria, kupanua ushirikiano na wananchi, kukuza na kudumisha demokrasia pamoja na mabadiliko ya Katiba.

Dar es Salaam. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimezindua mpango kazi wa miaka sita, huku kikieleza kuwa uchechemuzi wenye lengo la kuboresha  na kubadilisha sheria, kupanua ushiriki wa wananchi, kukuza na kudumisha demokrasia pamoja mabadiliko ya Katiba ni miongoni mwa maeneo yatakayofanyiwa kazi.

Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga amesema hayo leo wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya kituo hicho na ubalozi wa Sweden nchini.

Aliyataja maeneo mengine yatakayofanyiwa kazi katika mpango huo utakaoisha mwaka 2024 kuwa ni, kuujengea umma uwezo kuhusu haki za binadamu na kuimarisha utendaji kazi wa kituo hicho.

"Ndani ya mpango huu tutachochea maboresho ya sheria na sera zinazosimamia haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu. Tutadumisha haki za jamii na za kiuchumi  na kuhakikisha  kila mwananchi anaishi katika mazingira safi na salama," amesema.

Kuhusu makubaliano hayo, Henga ameishukuru Serikali ya Sweden kwa ushirikiano wa muda mrefu huku akisema yamekuja wakati muafaka ambao kituo hicho kimezindua mpango mkakati wa miaka sita.

Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg amesema Serikali ya nchi yake itaendelea kushirikiana na LHRC kwa kuwa imejitahidi kupigania utawala wa sheria  na kutetea haki za binadamu.

"Hii ni awamu nyingine ya ushirikiano wa muda kati ya ubalozi wa Sweden na LHRC. Haki ya kuishi, utu , uhuru, usawa, amani ni muhimu kwa kila mtu," amesema  Balozi Sjoberg.