Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pigo jingine kwa Clouds Media, Ephraim Kibonde afariki dunia

Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi, Ephrahim Kibonde.

 


Muktasari:

Clouds yapata pigo linguine, yampoteza mtangazaji wake mahiri na maarufu nchini, Ephrahim Kibonde aliyefariki dunia alfajiri ya leo akiwa hospitali ya Bugando


Siku chache baada ya kampuni ya Clouds Media Group kumpoteza Mkurugenzi wake wa vipindi na uzalishaji, Ruge Mutahaba imepata pigo lingine leo alfajiri ya Alhamisi Machi 7, 2019, baada ya kifo cha mtangazaji wa kipindi cha Jahazi, Ephrahim Kibonde.

Kibonde ambaye alikuwa MC kwenye msiba wa Ruge amekutwa na umauti kwenye hospitali ya Bugando mkoani Mwanza.

Mtangazaji huyo alikuwa miongoni mwa waombolezaji waliomsindikiza Ruge hadi katika maziko yake wilayani Bukoba.

Kwa mujibu wa Sebastian Maganga, taratibu zinafanyika kupanga mipango ya msiba huo.

“Ni pigo kubwa kwa familia ya Clouds Media Group, kwa familia ya Kibonde lakini kama tulivyoshikamana kwenye msiba wa Ruge, naomba tushikamane kwenye msiba huu,”amesema Maganga.