Soma jinsi kaswende inavyoua watoto wakiwa tumboni wakati wa ujauzito

Muktasari:

Tafita zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2016 ziliripotiwa kesi 661,000 za kaswende ya kurithi, kesi hizi zilisababisha vifo 200,000 vya watoto wakati wa kujifungua na wengi kabla hawajazaliwa.

Dar es Salaam. Je unafahamu kwamba kaswende ya kurithi (congenital syphilis) ni chanzo cha pili ulimwengenu kinachosababisha watoto kuzaliwa wakiwa waameshafariki?

Kwa mujibu wa taarifa zilizitolewa hivi karibuni na Shirika la Afya duniani (WHO), kaswende ya kurithi inafuatia baada ya malaria kama chanzo kikubwa cha vifo vya watoto kabla na wakati wa kuzaliwa.

Tafita zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2016 ziliripotiwa kesi 661,000 za kaswende ya kurithi, kesi hizi zilisababisha vifo 200,000 vya watoto wakati wa kujifungua na wengi kabla hawajazaliwa.

Kaswende ni moja kati ya magonjwa ya zinaa yanayoongoza ulimwenguni ikiwa na kesi mpya takribani milioni 6 kila mwaka.

“Endapo mama mjamzito aliambukizwa na hatopata matibabu madhubuti kwa wakati, anaweza kumuambukiza mtoto aliye tumboni, hii huitwa kaswende ya kurithi,” inaeleza taarifa hio ya shirika ya WHO.

 

Mbali na vifo, maambukizo hayo kwa watoto wachanga husababisha mtoto kuzaliwa na kilo ndogo sana au kuzaliwa njiti vilevile husababisha ulemavu.

Kaswende ya kurithi inaepukika kirahisi endapo mama mjamzito atagundulika mapema na kupewa tiba inayostahili. Wajawazito wenye kaswende hupatiwa dawa kama benzathine na penicillin kipindi cha mwanzo wa ujauzito.

Hii hupunguza kwa asilimia kubwa maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

WHO imetoa wito kwa mifumo yote ya afya kuhahakikisha kuwa wajawazito na vichanga wote wanaogundulika kuathirika na kaswende wanapatiwa matibabu stahiki na haraka iwezekanavyo.

“Vilevile kupunguza maambukizi ya kaswende, nchi zinatakiwa kuhakikisha kua kitendo cha kupima na kupatiwa matibabu kwa wenza kinafanyika katika kipindi chochote na sio kliniki tuu wakati wa ujauzito.