Ujumbe wa Mo Dewji wagusa wengi mtandaoni

Muktasari:

Mfanyabiashara Mohamed Dewji ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuandika ujumbe kuhusu anayekufanyia mabaya umlipe kwa mema na kuwagusa watu wa kada mbalimbali

Dar es Salaam. Ujumbe wa mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ aliouweka katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akizungumzia kutenda mema hata kama umefanyiwa ubaya umeibua mjadala mitandaoni.

Katika ujumbe huo Mo ambaye alitekwa na watu wasiojulikana Oktoba 11, 2018 na kupatikana  Oktoba 20, 2018 ameandika, “Hutofanya ubaya kwa aliyekufanyia ubaya, ila utamsamehe na kumfanyia ukarimu.”  Mtume Muhammad (S.A.W) JumaahKareem.

Baada ya ujumbe huo watu wa kada mbalimbali wametoa maoni yao akiwemo waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki aliyesema, “Hii ni imani ya ngazi ya juu sana.”

Wengine walioonyesha kuguswa na ujumbe huo ni @MsTayanah aliyeandika, “ila mkuu watanzania bado tungependa kujua walikupeleka wapi mkuu.”

Naye gagula16 ameandika, “Safi sana ndio maana halisi ya hekima. Na ndio maana mfalme Suleiman aliomba hekima na busara kwa mwenyezi Mungu.”

Naye MrMsambwe6% amesema, “Mungu akubariki katika kutufikishia ujumbe katika siku takatifu ya leo Nikutakie ijumaa Kareem.”

“Watu wakarimu tunalipizaga ubaya kwa wema mpaka  wanaona aibu,” amesema Bonimawalla.