Mapinduzi ya kidijatali yanaponya au yanaua?

Friday November 22 2019

 

By Ephrahimu Bahemu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Kwa miaka ya hivi karibuni hususani ndani ya karne ya 21 ni wakati ambapo dunia imeshuhudia mapinduzi makubwa katika teknlojia ya dijitali, unaweza sema zama za sasa ni za kidijitali.

Dijitali imekuja na mambo mengi mazuri kwa mabaya na mpaka sasa haijafahamika siku zijazo kipi kitakuwa kikubwa Zaidi katika faida na hasara zake lakini mpaka sasa faida zinaonekana kuwa nyingi zaidi hususani katika kuongeza ufanisi wa shughuli nyingi.

Wataalamu wengi wa teknolojia na watu wengine ambao wamewahi kuonja matunda ya dijitali wanasema haitoshi tu kuendesha maisha kwa utaratibu wa kale katika zama hizi kwani dijitali ina nafasi kubwa ya kufanya mabadiliko chanya katika taasisi yoyote ile hususani huduma na biashara.

Rais wa kampuni ya kiteknolojia ya Huawei Afrika Lu Baoqiang anasema kampuni zote zinapaswa kubadilika upesi na kuendana na teknolojia ya dijitali kwani kuna hatari kuwa ambazo hazitafanya hivyo zikapoteza malengo yake.

Alitolea mfano wa kampuni za simu akisema miaka si mingi iliyopita suala la kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi lilionekana kubadilisha sana dunia lakini hivi sasa data (internet) imechukua nafasi hiyo na jicho hivi sasa lipo katika eneo hilo.

“Ili kuendana na wakati huna budi ya kuendana na teknolojia iliyopo na kubadilika, na tunapozungumzia mageuzi ya kidijitali na juu ya namna ya kuhudumia wateja kwa nia rahisi ya kidijitali huku ukiboresha huduma unayowapatia,” anasema Baoqiang.

Advertisement

Anasema Huawei kwake mageuzi ya kidijitali ni uwezo mpya unaohusisha zama, majukwaa, mifumo ya uchakataji, oparesheni, muundo wa bidhaa na huduma ambazo zinaongeza mapato, ufanisi, kupunguza gharama na huduma nzuri kwa wateja.  

Huawei ambayo inafanya shughuli zake katika nchi Zaidi ya 170 duniani  inafanya kazi kwa karibu na kampuni za kiafrika kama Safaricom ya Kenya ambapo waliasaidia kunzishwa kwa mifumo madhubuti inayosimamia miamala katika simu.

Advertisement