Bashe: Hakuna nzige Tanzania

Thursday February 13 2020

 

By Habel Chidawali, Mwananchi [email protected]

Dodoma.  Naibu Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe amesema hakuna nzige walioingia Tanzania kama inavyodaiwa.

Amesema ikiwa wataonekana nchini watashughulikiwa kabla ya kuleta madhara kwa wakulima.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 13, 2020  wakati  akizungumza na wadau wa kilimo, mifugo na uvuvi katika kongamano  lililofanyika mkoani Dodoma.

Nzige walionekana kwa wingi nchini Kenya na hivi karibuni mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema walionekana mkoani humo, baadaye kutoweka kusikojulikana.

Amesema baada ya taarifa za nzige kuwa wamesogea katika ardhi ya Tanzania, Serikali ikipeleka wataalamu mipakani kwa ajili ya kufanya uchunguzi na taarifa inaonyesha hadi leo hakuna mahali walipoonekana

"Tumechukua hatua za kutosha kuhakikisha wanaoonekana katika ardhi yetu wanashughulikiwa kikamilifu bila kuleta madhara kwa wakulima wetu," amesema.

Advertisement

 

Advertisement