Hashim Kambi asema Richie Richie ni baba yake

Tuesday September 3 2019Msanii wa filamu nchini Tanzania, Hashim Kambi

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Hashim Kambi 

By Nasra Abdallah,Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Pamoja na kuwa mkubwa kiumri, Msanii wa filamu nchini Tanzania, Hashim Kambi amesema katika sanaa mtu anayemuheshimu na kumuona kama baba yake ni Richie Richie.

Kambi mwenye miaka 63 ameyasema hayo katika mahojiano maalum naMwananchi  alipokuwa akielezea safari yake ya sanaa hadi kufika hapo alipo.

Akielezea namna alivyounganishwa kwenye sanaa na Richie ambaye jina lake halisi ni Single Mtambalike, Kambi amesema siku moja akiwa katika shughuli zake za biashara alikutana na msanii huyo na kumueleza namna gani anapenda kuigiza.

“Nilimueleza Richie namna nilivyokuwa nikivutiwa na uigizaji wake na ule wakina Natasha na  Jacob Steven kwenye tamthiliya ya ‘Mambo Hayo’ hivyo nikamuomba kama naweza kupata nafasi ya kuigiza.”

“Richie kwa kuwa tulijuana kwenye mashabiki wa timu ya Yanga, nilipomwambia hivyo ilikuwa rahisi na hapo ndio akampigia simu baba Haji na kumueleza kuwa wamepata mtu wa kucheza nafasi ya Benjamini katika tamthiliya ya ‘Uhondo wa Ngoma,” amesema

Tamthiliya hiyo ilikuwa ikiigizwa na wasanii kutoka kundi la maigizo la Kamanda Arts Family chini ya uongozi wake Haji Adam maarufu ’Baba Haji’ na kurushwa katika kituo cha TVT enzi hizo ambapo kwa sasa inajulikana kwa jina la Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC).

Advertisement

“Humo nilipewa nafasi ya kucheza kama Mzee Benjamin  aliyekuwa tajiri katika hadithi ya tamthiliya hiyo na kujikuta nakuwa maarufu na kupata kazi nyingi za kufanya za filamu.

“Ni kutokana na Richie kunifungulia njia huko mpaka sasa hivi nimeweza kuwa msanii mkubwa na ninayeheshimika namshukuru kwa hilo na kwani huwa namuita baba yangu wa sanaa,” anasema Kambi.

 

Advertisement